Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Wabongo wanaponda sub za Amrouche'

Stars Weru Wabongo wanaponda sub za Amrouche

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau wanalalamika sana kuhusu mabadiliko ya wachezaji [substitutions] ambayo mwalimu aliyafanya. Wanalalamika baada ya Uganda kufunga goli na kupata alama tatu (3).

Pengine kama Uganda wasingefunga kusingekuwa na mtu wa kulalamika. Kuanzia dakika ya 65 Uganda waliongeza kasi ya mchezo, na kwa namna mechi ilivyokuwa huwezi kushangaa kwa nini ilikuwa hivyo!

Ilikuwa ni mechi ya Fainali kwa Uganda, wanegepoteza mechi ile maana yake wangekuwa nje ya mashindano. Mpira jinsi ulivyo, kucheza dhidi ya timu ambayo haina cha kupoteza ‘kujilipua’ ni ngumu sana.

Kadiri muda ulivyozidi kuwa unaenda Taifa Stars walihitaji walau alama moja kwenye mchezo wa jana ili kufikisha alama tano (5) ambapo kama ingeshinda mechi inayofuata dhidi ya Niger inefikisha alama nane (8) na kujihakikishia kufuzu.

Ukisikia wadau utasikia wanalalamika kwa nini Mzamizu alitolewa wanasahau kuwa tayari alishafabya kazi kubwa na kutumia nguvu nyingi. Mwalimu akaona ni bora aingie mtu ambaye atakuwa na nguvu mpya.

Himid Mao aliumia na ilikuwa ni 50/50 kucheza hata hiyo mechi ya jana! Lakini alikomaa kapigana, ikafika wakati ukimtazama anaonekana anahitaji kupumzika.

Samatta pia alikimbia sana na kuwakaba mabeki wa Uganda, kwa hiyo ilifika wakati anahitajika mchezaji mpya ili kuendelea kufanya pressing kwa mabeki.

Lakini matokeo ya mpira wakati mwingine yanashangaza! Sekunde kadhaa nyuma hakuna mtu alikuwa anafikiria Uganda watafunga goli. Nafasi ikapatikana likafungwa goli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live