Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabongo waivamia Mamelodi Sundowns

Dds Yanga Mamelodi Wabongo waivamia Mamelodi Sundowns

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Mamelodi Sundowns kuweka post kuwa watacheza na Yanga SC kwenye hatua ya robo fainal ya CAFCL, mashabiki wa mpira wa miguu Tanzania wamevamia ukurasa wa Instagram wa Mamelodi kwenye post zilizopostiwa jana na asilimia 90 ni comment kutokea Bongo.

Si post hiyo, hata post za kabla ya droo hiyo kuchezeshwa na kupangwa mechi za robo fainali, hata post za baadaye, mashabiki wa Bongo hususani Yanga wameonekana ku-comment kwa Kiswahili wakiwachimba mkwara Masandawana kuwa Yanga iko vizuri na itawafanya kitu kibaya wenye hatua hiyo ya robo fainali.

Mchezo wa kwanza kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi umepangwa kuchezwa katika Dimba la Mkapa kati ya Machi 29-31 kabla ya kurudiana nchini Afrika Kusini wiki moja baadaye.

Mmoja wa mashabiki wa Mamelodi ameonesha kutoelewa lugha inayoandikwa kwenye ukurasa huo (Kiswahili) huku akionesha wasiwasi kuwa imeibiwa (hacked).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live