Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabongo waishika Nairobi mapemaaaa

69817 Wabongo+pic

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

NAIROBI. WAKATI zikibaki saa tano (5) kabla ya mechi ya marudiano baina ya timu ya Taifa ya Kenya na Tanzania 'Taifa Stars' jijini hapa, kundi la mashabiki wa soka kutoka Tanzania limegeuka kivutio mitaa ya jiji hilo.

Kundi hilo maarufu kama Taifa Stars Supporters limeanza kuonyesha mfano wa kile ambacho kitaenda kufanyika uwanjani baadaye katika mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Kasarani.

Mashabiki hao wamekuwa wakishangilia kwa kupiga ngoma na kucheza tangu nyakati za saa 5 asubuhi wakati wakijiandaa kwenda kwenye hoteli ambayo Taifa Stars wamefikia jijini hapa.

Mbwembwe za uchezaji wa mashabiki hao zimewafanya baadhi ya Wakenya ambao wanafanya shughuli katika maeneo hayo, kujazana na kuwatazama.

Mechi hiyo baina ya Kenya na Taifa Stars ni ya marudiano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (Chan).

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare tasa.

Chanzo: mwananchi.co.tz