Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wababe wa Yanga waua CAF, Makambo aibeba Horoya kwa Enyimba

97624 Makambo+pic Wababe wa Yanga waua CAF, Makambo aibeba Horoya kwa Enyimba

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wababe wa Yanga, Pyarmids ya Misri wameendeleza moto wao katika mechi ya Kombe la Shirikisho baada ya jioni hii kuipasua Zanaco ya Zambia kwa mabao 3-0, huku Horoya AC ya Herritier Makambo aliyewahi kukipiga Jangwani wakilazimisha sare ugenini dhidi ya Enyimba.

Pyramids walioing'oa Yanga kwenye play-off kuwania kutinga makundi ya michuano hiyo hivi karibuni kwa kuwafunga nje ndani kwa jumla ya mabao 5-1, walipata ushindi mjini Lusaka katika mechi yao ya kwanza ya robo fainali kwa mabao ya Ali Gabr dakika ya 18 akimaliza kazi nzuri ya nahodha wake, Abdallah Said kabla ya dakika sita baadaye Mohammed Faroukh kufunga la pili.

Abdallah Said ambaye ni mmoja ya wachezaji walioitesa Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na baadaye katika mechi ya marudiano nchini Misri, alifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 68 na kuwapa ushindi matajiri hao wanaoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Kwenye mchezo mwingine wa michuano hiyo, Enyimba ya Nigeria wakiwa nyumbani walitoshana nguvu na Horoya AC ya Guinea kwa kufunga bao 1-1, huku nyota wa zamani wa Yanga, Makambo akiingizwa uwanjani kipindi cha pili katika pambano hilo.

Bao la wenyeji liliwekwa kimiani na Augustine Oladapo dakika ya 18 kabla ya Horoya kuchomoa dakika ya 71 kupitia Boniface Haba muda mchache tangu Makambo na Tafadzwa Kutinyu aliyekuwa akiichezea Azam FC kuingizwa uwanjani kuchukua nasi za Aristide Bance na Morlaye Sylla dakika ya 60 na 66 na kuichangamsha safu ya ushambuliaji ya wababe hao wa Guinea.

Muda mchache baadaye kwenye mfululizo wa mechi hizo, Al Nasry ya Libya na Hassania Agadir ya Morocco, huku El Masry ya Misri wakivaana na Berkane pia ya Morocco.

Pia Soma

Advertisement

 

Chanzo: mwananchi.co.tz