Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wababe Championship kuendelea kuumiza nyasi

Pamba Jiji Fc Sq Kikosi cha timu ya Pamba Jiji

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya leo kushuhudiwa mchezo mmoja ukipigwa kati ya wenyeji Mbeya City inayoikaribisha Pamba Jiji kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kuanzia saa 10:00 jioni, Ligi ya Championship inaendelea tena kesho kwa mzunguko wa 10 ambapo timu tano zitakuwa zikisaka pointi tatu.

Mchezo wa mapema utakaochezwa saa 8:00 mchana utazikutanisha Ruvu Shooting iliyotoka kuchapwa mabao 3-1 na Pamba Jiji katika mechi iliyopita, itaikaribisha Biashara United kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ikiwa na kumbukumbu ya kuichapa Mbeya City 2-1.

Copco iliyotoka kuchapwa mabao 2-1 na Mbeya Kwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kucheza na KenGold, huku ‘Chama la Wana’ Stand United ikiwa na kibarua kigumu kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza.

TMA iliyoifunga Transit Camp kwa bao 1-0, katika mchezo uliopita itakuwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kucheza na Polisi Tanzania iliyotoka kuifunga Pan Africans mabao 2-0, huku Cosmopolitan ikiikaribisha Green Warriors katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa kwa michezo miwili pia kupigwa ambapo Mbuni itakuwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kucheza na FGA Talents huku Pan Africans ikiwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kupambana na Transit Camp.

Akizungumza Kocha Mkuu wa Copco, Feisal Hau amesema awali ushindani ulikuwa unaonekana mwishoni mwa msimu, lakini msimu huu mambo ni tofauti kwani kila timu inahitaji kukusanya pointi nyingi mapema ili kupunguza presha mbeleni.

“Haina maana kwamba unapoanza vizuri basi utamalizia hivyo hivyo, isipokuwa unapokusanya pointi nyingi mapema inakuwa afadhali. Msimu huu umekuwa mgumu kwa sababu hakuna pengo kubwa kati ya timu inayoongoza na iliyopo nafasi ya 10,” amesema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti