Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu wavuruga dili la Amrabat kwenda Man United

Sofyan Amrabat To Atletico Kiungo wa Fiorentina, Sofyan Amrabat

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Manchester United kuonekana ipo kwenye hatua nzuri kuipata huduma ya kiungo wa Fiorentina, Sofyan Amrabat, 26 taarifa zinadai dili hilo huenda likapinduka muda wowote kuanzia sasa baada ya matajiri wa Al Hilal kuanza mazungumzo na wawakilishi ili wamsajili katika dirisha hili.

Taarifa zinaeleza kwamba dili hilo linaweza kugeuka kwa sababu AlHilal wamepanga kumuwekea mshahara mnono zaidi fundi huyu na kumalizana na Fiorentina mapema kwenye masuala ya ada ya uhamisho.

Man United ambayo ndio ilikuwa ya kwanza kwenye harakati za kuiwania huduma ya fundi huyu imekuwa ikisuasua kwenye masuala ya ada ya uhamisho kutokana na bajeti yao katika dirisha hili kuwa ndogo.

Hata hivyo, mashetani wekundu wana jeuri kwamba watampata Amrabat kwa sababu staa mwenyewe ameonyesha kupendezwa na mipango yao na amekuwa kwenye mawasiliano ya karibu na kocha wao Erik Ten Hag.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live