Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu wapania kuibomoa Man United

Bruno Fernandez Ww Kiungo wa Ureno, Bruno Fernandes

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inadaiwa kuwa nahodha wa ‘klabu’ ya Manchester United, Bruno Fernandes, ni kivutio cha ‘klabu’ mbalimbali kutoka nchini Saudi Arabia, na inaelezwa kuwa wawakilishi kutoka PIF, wamiliki wa klabu za Al Hilal, Al Nassr, Al Ahli na Al Ittihad wanataka kufanya mazungumzo na wakala wa kiungo huyo juu ya uwezekano wa kumsajili msimu ujao.

Iwapo uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 kwenda nchini humo utakamilika, basi atajiunga na wachezaji wengine kama, Cristiano Ronaldo, Sadio Mane, Karim Benzema na Riyad Mahrez waliojiunga kutokea Ligi Kuu England.

Pia ‘klabu’ za Saudia zinawafuatilia kwa ukaribu mchezaji wa ‘klabu’ ya Liverpool, Mo Salah pamoja na kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live