Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu wanavyopigana vikumbo kumpa utajiri Salah

Mo Salah S Winga wa Liverpool, Mohamed Salah

Mon, 5 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kushindikana kutua Saudi Arabia dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, bado timu kutoka nchi hiyo zinatamani kumsajili staa wa Liverpool, Mohamed Salah dirisha hili na taarifa zinadai kuna uwezekano mkubwa akakamilisha dili hilo.

Salah ameahidiwa mshahara wa zaidi ya Pauni 60 milioni kwa mwaka ikiwa atajiunga na timu hiyo. Kiasi hicho cha pesa kitamfanya kuwa tajiri maradufu zaidi kutokana na utajiri ambao yupo nao kwa sasa.

Hapa tumekubainishia mali na pesa ambazo staa huyu anazo na jinsi anavyoweza kutajirika zaidi ikiwa atatua Saudia.

ANAPIGAJE PESA?

Staa huyu ambaye ana utajiri unaofikia Dola 90 milioni, alianza kupiga pesa baada ya kujiunga na Chelsea mwaka 2014 na alikuwa akilipwa Pauni 65,000 kwa wiki, zaidi ya Pauni 3.12 milioni kwa mwaka na pamoja na bonasi ilifika Pauni 4 milioni kwa mwaka.

Kwa sasa akiwa na Liverpool anakunja Pauni 350,000 kwa wiki ambazo hufikia Pauni 18 milioni kwa mwaka.

Mbali na pesa hizo anazopiga kupitia mishahara yake na Bonasi, pia ana madili kibao aliyosaini na kampuni kubwa duniani kama balozi wao.

Kwa sasa ana mkataba na Adidas akitamngaza kampuni hiyo kwa kuvaa viatu vyao awapo uwanjani.

Pia ana mkataba na kampuni ya Vodafone ya Misri, Uber pamoja na Pepsi ambayo alisaini nao mkataba tangu mwaka 2016.

Kutokana na kampuni hizo, anapata jumla ya Dola 5 milioni kwa mwaka, pamoja na pesa nyingine zitokanazo na matangazo mbalimbali kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

MCHANGO WAKE KWA JAMII

Ni mmoja wa watu wanaojitoa kwenye jamii na mwaka 2019 alitoa Dola 3 milioni kwa taasisi inayojishughulisha na masuala ya Kansa Oman, ili kusaidi mchakato wa kununua vifaa baada ya majambazi kuvamia na kuondoka na vifaa.

Pia Salah ni balozi wa Shirika la afya Duniani UNHCR na mmoja ya wadau wakubwa wa kusaidia watoto yatima na watu wasiojiweza akiwa na taasisi yake ya Mohamed Salah Charity Foundation.

NDINGA

1. Lamborghini Aventador-Dola 507,353

2. Mercedes-Benz GLE Coupe-Dola 89,800

3. Porsche 911 Turbo S-Dola 273,750

4. Bentley Bentayga-Dola 339,150

5. Audi Q7-Dola 61,795

6. Bentley Continental-Dola 270,150

MJENGO

Ana mjengo wa kifahari jijini Liverpool wenye thamani ya Pauni 4 milioni, kwa mujibu wa Salah mwenyewe, nyumba hiyo ina vyumba viwili kwa ajili ya Salah kufanya mazoezi.

Mbali ya vyumba vya kulala, nyumba hiyo ina bwawa la kuogelea na sehemu ya kuchezea soka vitu vinavyompa staa huyo kuwa na nafasi ya kufanya mazoezi na kutulia akiwa mjengoni bila ya kwenda kokote katika siku zake za mapumziko.

MAISHA NA BATA

Jina lake kamili ni Mohamed Salah Ghaly alizaliwa Juni 15, 1992 kwa sasa ana umri wa miaka 27. Yupo kwenye ndoa na mwanadada Maggi tangu Desemba 17, 2013 na kupata watoto wawili, Makka na Kayan Salah.

Kuhusu suala la bata jamaa sio mtu wa mambo hayo kabisa, muda mwingi wa mapumziko huwa anautumia kukaa na familia na hata anapotoka huwa pamoja na familia yake.

Chanzo: Mwanaspoti