Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu wamerudi tena mawindoni

Richarlison Saida Mshambuliaji wa Spurs, Richarlison

Tue, 14 May 2024 Chanzo: Dar24

Mabingwa wa Ligi Kuu Saudi Arabia, AHilal wana matumaini makubwa ya kuipata saini ya Mshambuliaji kutoka nchini Brazil na Klabu ya Tottenham, Richarlison de Andrade dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Matumaini ya matajiri hao yametokana na mazungumzo iliyofanya na wawakilishi wa mchezaji na Richarlison mwenyewe na wote wameonyesha kuhitaji kukamilisha dili hilo.

Richarlison mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akiwindwa na timu kibao za Saudia tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana baada ya mwenyewe kukataa.

Kwa sasa anaonekana kuwa tayari kutimkia huko na taarifa kutoka The Fooball Insider zinaeleza Spurs inaweza kumsajili Eberechi Eze dirisha lijalo ili akacheze kama mbadala wa Richarlison.

Ikiwa Spurs itamuuza staa huyu, itapata zaidi ya Pauni 80 milioni wakati Richarlison mwenyewe atapata mshahara wa Pauni 12 milioni kwa mwaka ambao ni mara tatu zaidi ya ule anaoupata kwa sasa.

Chanzo: Dar24