Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu waitumia Yanga kuimaliza Simba

Simba Wydad Gd Waarabu waitumia Yanga kuimaliza Simba

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wapinzani wa Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad Casablanca kutoka Morocco, wamepanga kuutumia mchezo wa Kariakoo Dabi kusoma zaidi mbinu za Simba kabla ya kukutana kwenye mchezo war obo fainali.

Katika kufanikisha hilo, Waarabu hao wana siku nne tangu watue hapa nchini kwa ajili ya kuwafuatilia kwa ukaribu Simba ambao Aprili 16, mwaka huu, watapambana na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba imepangwa kucheza dhidi ya Wydad Casablanca katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mchezo wa kwanza ni Aprili 21 jijini Dar, kisha marudiano Aprili 28, nchini Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Simba ina taarifa za ujio wa siri wa Wydad ambao wapo tangu Ijumaa iliyopita wakiwafuatilia kila hatua wanayoipiga.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa makachero hao wa Wydad Casablanca tayari wamewaona Simba katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports waliocheza dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar ambao Simba ilishinda 5-1.

Aliongeza kuwa, makachero hao wamepanga kuungalia mchezo wa Kariakoo Dabi utakaozikutanisha Simba dhidi ya Yanga utakaopigwa Aprili 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

“Baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wydad Casablanca wapo hapa nchini tangu wiki iliyopita wakiifutilia Simba.

“Mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi utakaowakutanisha Simba dhidi ya Yanga, wataondoka wakiwa na mafaili yote ambayo watakayakabidhi kwa benchi lao la ufundi.

“Kama uongozi tulifahamu hilo, hivyo hatuna hofu kwani na sisi tumepanga kuwawahisha viongozi wetu huko Morocco kwa ajili ya kuwafuatilia wapinzani wetu hao.

“Hiyo haitufanyi tuwaogope na badala yake tunaendelea na maandalizi yetu kwa ajili ya mchezo huo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa: “Tunafahamu kila kitu kinachoendele, kama uongozi kila mchezo uliopo mbele yetu tunauchukulia kama fainali.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live