Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu wafanya kufuru kwa Ederson

Skysports Man City Ederson 5602425 Golikipa wa Man City, Ederson

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester City imepokea ofa ya Pauni 25 milioni kutoka kwa Al Nassr ya Saudi Arabia kwa ajili ya Ederson ambayo mbali ya kutoa pesa hiyo kwa ajili ya kuvunja mkataba wake, pia imemwekea kipa huyo ofa ya mshahara mnono wa Pauni 900,000 kwa wiki.

Kipa huyu wa kimataifa wa Brazil mkataba wake na Man City unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu uliopita alicheza mechi 43 za michuano yote na kufungwa mabao 34.

Ederson anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kujiunga na matajiri hawa kutokana na kiasi cha pesa alichowekwa na umri wake ambapo kwa sasa ana miaka 30.

Kipa huyu ambaye ameshinda karibia kila taji kwa ngazi ya klabu mshahara wake wa sasa ni Pauni 100,000 kwa wiki sawa na Pauni 5.2 milioni kwa mwaka.

Ikiwa atatua Al Nassr ataweza kupata pesa ya mwaka ndani ya mwezi mmoja na nusu tu.

Wakati huo huo, Manchester United ipo tayari kumuuza beki wao kutoka Sweden Victor Lindelof, 29, anayehitajika na Fenerbahce pamoja na kiungo kutoka Denmark, Christian Eriksen katika dirisba hili.

Eriksen na Lindelof hawaonekani kuwa katika mipango ya Erik ten Hag kwa msimu ujao, mkataba wa Lindelof unamalizika mwaka 2025. wakati ule wa Eriksen ukimalizika mwaka 2025.

CHELSEA ipo tayari kupambana na Tottenham, Bayern Munich na Paris St-Germain kwa ajili ya kuiwania saini ya kiungo wa Rennes na Ufaransa Desire Doue, katika dirisha hili.

Doue alionyesha kiwango bora kwa msimu uliopita kiasi cha kuvutia timu nyingi barani Ulaya zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili. Doue mwenye umri wa miaka 19, mkatana wake unamalizika mwaka 2026.

KIPA raia wa Denmark, Kasper Schmeichel yupo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kujiunga na Celtic katika dirisha lijalo.

Kasper ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kuachana na Anderlecht katika dirisha hili, alifanya vipimo vya afya wikiendi iliyopita.

BEKI wa zamani wa Manchester United, Raphael Varane yupo katika hatua za mwisho kusaini mkataba wa kujiunga na Como ya Serie A akiwa huru baada ya kumaliza mkataba wake na Man United mwezi uliopita.

Kumekuwa na timu nyingi zinazohitaji saini ya Varane hususani ambapo mbali ya zile zilizopo barani Ulaya kuna ofa pia kutoka Saudi Arabia.

WEST Ham imevutiwa na winga wa Ajax na Uholanzi Steven Bergwijn, 26, na inataka kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili lakini kuna upinzani mkubwa kutoka kwa Marseille na timu mbili kutoka Saudi Arabia ambazo zinahitaji huduma yake.

Steven ambaye msimu uliopita alicheza mechi 31 za michuano yote na kufunga mabao 13, mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

ATLETICO Madrid ipo tayari kumruhusu straika wao Alvaro Morata, 31, kujiunga na AC Milan au timu yoyote atakayohitaji katika dirisha hili kuanzia wiki ijayo.

Morata ambaye ni kapteni wa timu ya taifa ya Hispania ameweka wazi kwamba hajisikii furaha kucheza Hispania kama akiwa anacheza nje ya nchi hiyo. Mkataba wa Morara na Atletico unamalizika mwaka 2026.

Chanzo: Mwanaspoti