Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu waandaa mpango maalum kuwavuta Salah, KDB

Salah X KDB Waarabu waandaa mpango maalum kuwavuta Salah, KDB

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu za Saudi Arabia zimeripotiwa kuwa na mpango maalumu wa kuwanasa masupastaa Mohamed Salah wa Liverpool na Kevin De Bruyne wa Manchester City itakapofika 2025.

Klabu za Saudi Pro League zinahaha kunasa mastaa wenye majina makubwa ili kuimarisha ligi yao kabla ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia 2034.

Kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, klabu za Saudi Arabia zilitumia pesa nyingi kunasa mastaa wenye majina makubwa kama Riyad Mahrez, Fabinho, N’Golo Kante, Aymeric Laporte, Ruben Neves na Aleksandr Mitrovic kwa kuwataja wa uchache.

Ligi hiyo pia inachezewa na mastaa wenye majina makubwa kama Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Mbrazili, Neymar.

Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi klabu hizo za Saudi Arabia zinaona kutakuwa na ugumu katika kuwapata Mo Salah na De Bruyne, lakini zinaamini kwamba itakapofika majira ya kiangazi mwakani, watanasa saini zao kirahisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live