Makamu wa rais wa Al Ittihad Jeddah Ahmad Essam Kaaki ameanza kumfuata (Kufollow) Mohamed Salah kwenye Instagram ili kuongeza ukaribu huku mazungumzo yakiendelea kimyakimya.
Awali vyombo vya habari vya Saudi viliripoti wiki iliyopita kwamba The Tigers wanataka kuweka mezani ofa ya pauni milioni 60 (£180m katika misimu miwili).
Kisha wakala wa Salah, Ramy Abbas, aliwahakikishia mashabiki wa Liverpool kupitia Twitter (sasa X) kwamba Mo anabaki.
Lakini asubuhi ya leo, ‘ombi la mashabiki wa Ittihad ni Salah’ lilisambaa kwenye X muda mfupi baada ya hapo, Makamu wa Rais wa klabu alimfuata Salah kwenye IG.
Na kisha, chombo maarufu cha habari cha Qatar Alkass kilidai Salah ameipa Ittihad ruhusa kuanza mazungumzo na Liverpool.