Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu kumng'oa Alisson Becker Liverpool

Alisson Becker Alisson Becker, 31

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Saudi Arabia sasa wamemjumuisha kipa Alisson Becker, 31, katika orodha ya wachezaji inayowahitaji kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi kutoka Liverpool.

Awali mchezaji aliyeonekana kuhitajika pekee kutoka Liverpool kwa dirisha lijalo alikuwa ni Mohamed Salah lakini sasa Becker naye anawindwa.

Mkataba wa kipa huyo wa kimataifa wa Brazil unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na hadi sasa haijajulikana ikiwa Liverpool itakuwa tayari kumuuza au laa kutokana na umuhimu wake katika timu.

Waarabu pia wanahusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Mohamed Salah ambaye imekuwa ikimuwinda katika dirisha lililopita lakini haikufanikiwa.

Moja ya sababu za Becker huenda akaondoka ni baada ya Kocha Jurgen Klopp kusema ataondokamwisho wa msimu, ingawa vyanzo vinaeleza hata kama ataondoka itahitajika kiasi kikubwa sana cha pesa kwa ajili ya kuwashawishi Liverpool ikubali kumuuza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live