Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waarabu kuibomoa Liverpool

Beeker Liverpool.png Waarabu kuibomoa Liverpool

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda Lango wa Liverpool, Alisson Becker anadaiwa hana mpango wa kuondoka kwenye kikosi cha ‘Majogoo wa Jiji’ licha ya kuwepo kwa ofa kutoka Al Nassr ambayo inataka kumsajili katika dirisha hili.

Inadaiwa Al Nassr inamtumia Mshambuliaji wao, Sadio Mane ili amshawishi Becker akubali kutua kwenye kikosi hicho kutokana na uhusiano wa karibu ambao wawili hao walikuwa nao wakati Mane akiitumikia Liverpool.

Becker ambaye anapokea mshahara wa Pauni 150,000 kwa juma anadaiwa atalipwa mara tatu zaidi ya pesa hiyo ikiwa atakubali kutua SaUdi Arabia.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya vigogo wa Al Nassr na Becker zaidi wawakilishi wake ndio wanaofanya mazungumzo.

Kipa huyu wa kimataifa wa Brazil ana mkataba na Liverpool hadi mwaka 2027, hali inayotia ugumu mwingine kwa Al Nasser ikiwa itataka kuuvunja.

Ikiwa kipa huyo atakubali atakuwa mchezaji wanne wa Liverpool kwenda Saudia baada ya Fabinho, Jordan Henderson na Firmino.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: