Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamana nyumbani kwa Netanyahu wakitaka vita isitishwe

Maandamano Netanyahu Waandamana nyumbani kwa Netanyahu wakitaka vita isitishwe

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa Israel wamemiminika mitaani kuitaka serikali yao kusitisha 'umwagaji damu' na kufikia makubaliano na Hamas ili kuwarejesha mateka.

Ndugu wa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na kundi la Hamas waliingia barabarani leo Alhamisi (Mei 2) kuishinikiza serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi hilo ili kurejeshwa kwa mateka wanaoshikiliwa.

Katika mji mkuu,Tel Aviv, waandamanaji waliweka vizuizi kwenye barabara kuu nyakati za asubuhi, huku wakipiga mayowe ya kutaka makubaliano ya haraka ili kukomeshwa kile walichosema ni 'umwagaji damu' na kuwarejesha mateka wote nyumbani.

Wengine walikusanyika mbele ya nyumba ya Netanyahu kuwasilisha ujumbe wao.

Mmoja wao alikuwa ni mama aliyebeba picha ya mtoto wake wa kiume, ambaye bado anashikiliwa mateka mikononi mwa Hamas.

Mama huyo alisema yeye na familia yake wako kwenye hali mbaya sana kama walivyo maelfu ya raia wengine wa Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live