Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi wapewa onyo zito

Refarees waamuzi walioshiriki maafunzo

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Siku chache baada ya waamuzi wa soka visiwani Pemba kupewa mafunzo maalumu kwa ajili ya Ligi Kuu ya Zanzibar, Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), limesema halitamvumilia mwamuzi yeyote atakayeshindwa kuzifuata sheria 17 za soka.

Katibu Msaidizi wa ZFF, Khamisi Hamad Juma ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waamuzi katika uwanja wa michezo wa Gombani visiwani hapa.

Amesema waamuzi wana jukumu la kuhakikisha wanatenda haki katika utoaji wa uamuzi ili kupunguza malalamiko yanayojitokeza viwanjani ambayo yanaweza kusababisha migongano isiyo ya lazima.

Hamad amesema msimu huu utakuwa ni tofauti na misimu iliyopita kwani ZFF watakuwa wakali kwa mwamuzi atakayekwenda kinyume na mafunzo waliyopewa hivi karibuni.

Amesema katika msimu uliopita waamuzi walikuwa wanalalamikiwa na viongozi na mashabiki wa timu kutokana na utoaji uamuzi usio sahihi wanapokuwa kwenye majumu yao.

“Nawaombeni waamuzi muwe makini wakati ligi itakapoanza kwani mara hii shirikisho halitamuonea huruma mwamuzi atayeshindwa kuzitafsiri ipasavyo sheria 17 za soka,” amesema Khamis.

Waamuzi wa soka, Said Salum na Suleiman Khatib walimhakikishia katibu huyo kuwa kutokana na mafunzo waliyoyapata watafanya kazi zao kwa weledi.

Hata hivyo, waliiomba ZFF kulipa uzito suala la ulinzi na usalama viwanjani kutokana na baadhi ya timu na mashibiki kujihusisha na masuala ya uvunjifu wa amani hasa timu zao zinapofungwa.

Chanzo: Mwanaspoti