Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi waliosimamishwa kufikiriwa

Arajiga Pic Data Waamuzi waliosimamishwa kufikiriwa

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ipo kwenye mchakato wa kuwaombea nafasi ya kuchezesha mechi za Ligi Kuu waamuzi zaidi ya 20 waliokuwa wamesimamishwa msimu uliopita.

Waamuzi hao walisimamishwa kutokana na sababu mbalimbali za kinidhamu na kikanuni hivyo kushindwa kumalizia ratiba zao kama walivyokuwa wamepangwa.

Miongoni mwa waamuzi hao ni Ahmed Aragija, Elly Sasii, Emmanuel Mwandembwa, Hussein Athman, Nassoro Mwin-chui, Florentina Zablon, Amina Kyando, Raphael Ikambi, Jackson Palangyo na Hans Mabena Wengine ni Rashid Zongo, Kassim Mpanga, Frednand Chacha, Sudi Lila, Herbeth Malime, Ahmed Simba, Marry Mwakitalama, Hamis Chang’aru na Jesse Erasmo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassoro Hamduni amesema jukumu lao ni kuwasaidia waamuzi katika changamoto wanazokutana nazo sehemu ya kazi lakini wao sio wenye maamuzi ya mwisho kwa mwamuzi ambaye amefungiwa kumrudisha kazini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: