Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi walevi wapoteza shavu UEFA

Waamuzi Walevi Waamuzi walevi wapoteza shavu UEFA

Thu, 8 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Waamuzi wa Uefa, Bartosz Frankowski na Tomasz Musial wameondolewa katika ratiba ya kuchezesha mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati ya Dynamo Kyiv na Rangers huko Poland baada ya kuripotiwa walikesha usiku kucha wakiwa wanalewa siku moja kabla ya mechi husika.

Kilichotokea ni, ndani ya saa 24 kabla ya mechi hiyo, wawili hao walisimamishwa kutokana na tabia ya ulevi wakidaiwa kulewa siku moja kabla ya mechi.

Mbali ya kulewa, pia walikamatwa na polisi wakiiba alama za barabarani ikiwa ni kutokana na kulewa kwao, inaripoti tovuti ya TVP Sport.

Baada ya kukamatwa na polisi, wawili hao walipelekwa katika kituo cha kutuliza akili ambako waliswekwa usiku kucha ili kusubiria pombe ziwaondoke.

Vituo vya kutuliza akili ni jambo la kawaida sana nchini Poland, na wastani wa watu 300,000 hukaa humo kwa mwaka na huwa inajumuisha watu mbalimbali ikiwemo na wale walevi waliokamatwa na polisi, pengine wakiwa wanaendesha ama wanafanya vitendo visivyofaa.

Baada ya kufikishwa hapo, inapofikia asubuhi na mtu akili zake zikawa sawa huwa wanaachiliwa lakini hutakiwa kulipa kiasi cha pesa.

Mchezo huo uliopigwa juzi na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, umefanyika katika Jiji la Lublin badala ya Kyiv kwa sababu za kiusalama kutokana na mgogoro unaoendelea huko Ukraine.

Baada ya mechi hiyo ya mkondo wa kwanza, Rangers itakuwa mwenyeji wa Dynamo huko Glasgow Agosti 13.

Mshindi wa mechi jumla katika mechi hii atafuzu kwenda raundi nyingine ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa.

Chanzo: Mwanaspoti