Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi wa Bongo katika ramani ya Soka Afrika

WAMUZI BONGO AFRIKA Waamuzi wa Bongo katika ramani ya Soka Afrika

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Cameroon inaibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Mauritius kwenye uwanja wa Omnisport uliopo Douala nchini Cameroon, November 17.

Pilato wa mechi hiyo alikuwa mwamba kutoka kwenye ardhi ya Nyerere Ahmed Aragija.

Pengine Aragija ni miongoni mwa waamuzi wanaofanya vizuri zaidi nchini kwasasa kwa ubora wa maamuzi yao.

Mwamuzi msaidizi namba moja alikuwa Frank Komba na ubavu wa namba 2 alikuwepo Kassim Mpanga halafu mezani alikuwepo mzee wa mikwara mingi Ramadhan Kayoko.

Hii ni hatua kubwa ambago tunaipiga kama Taifa kwasasa kwenye upande wa waamuzi. Miaka kadhaa nyuma hatukuwahi kuwa na waamuzi katika hatua kama hizi na hata tulipobahatika tukatoa mmoja pekee lakini sasa safu nzima inatoka Tanzania maendeleo makubwa sana haya.

Pengine hili linaweza kupunguza makosa kwa waamuzi wetu na kuwafanya watende kwa weledi mkubwa wakijua wanafuatiliwa kwa ukaribu mkubwa.

Sasa ni jukumu letu kama watanzania kuwapa nguvu na kuwapunguzia presha zinazowafanya watende maamuzi yenye utata.

All the best Champions naimani wakati mwingine tena tutatoa waamuzi wengi zaidi wataochezesha michuano mikubwa....

Tuendelee kuwakubali manabii wetu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live