Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi ndio sababu Pablo "kumind" mabadiliko ya Wawa

Pablo Hasira Pablo Franco Martin

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba SC, Pablo Franco ameelezea kitendo kilichopelekea kuonesha Jazba Uwanjani jana wakati wa mchezo kati ya Simba na KMC.

Pablo amesema kilichomfanya awe na Jazba ni mapungufu ya waamuzi wakati wa kufanya Mabadiliko.

“Kilichotokea ni kwamba tuliomba kufanya mabadiliko na kulikuwa na wachezaji wawili tayari, mwamuzi wa mezani alikua ana majina mawili yanayofanyiwa mabadiliko kwa wakati mmoja, kama mnavyojua kuna madirisha matatu tu ya kufanya mabadiliko kwenye mchezo kwa Wachezaji watano.”

Pablo ameeleza kuwa waamuzi waliruhusu mchezaji mmoja kuingia uwanjani wakati wao waliomba kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili.

“Tulishatumia dirisha la kwanza, tulikua tunaenda kutumia dirisha la pili kwa wachezaji wawili tukiwa tumebakiwa na dirisha moja la tatu kabla ya mchezo kuisha. Sijui kwa nini mwamuzi aliruhusu mchezaji mmoja tu kuingia na sio mchezaji wa pili kwa hivyo tulikua tunapoteza dirisha moja.”

“Kosa lilikua kubwa sana kwa faida ya wachezaji wetu. Ndio maana nilipata hasira sana.”

Aidha, ameomba radhi kwa waamuzi na mashabiki kutokana na kitendo hicho kwani si cha kiungwana.

Kitendo kilichotokea katika mchezo siku ya jana kilizua taharuki kwa wapenzi na Mashabiki wa soka nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live