Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi Simba, Yanga wapewa Kombe la Dunia

Waamuzi Kombe La Dunia Waamuzi Simba, Yanga wapewa Kombe la Dunia

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemtangaza waamuzi watakao chezesha Kombe la Dunia chini ya umri wa 18 yatakayofanyika nchini Argentina kuanzia Mei 20-11 Juni mwaka huu.

Waamuzi watakaochezesha mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Wydad Casablanca Issa Sy kutoka Senegal, na wasidizi wake Bongoura Nouha kutoka Senegal, Desire Ngoh wa Ivory Coast wamechaguliwa kuchezesha pia Kombe la Dunia.

Rekodi zinaonyesha katika michezo 16 aliyochezesha refa huyo, timu za nyumbani zimeshinda mechi 10, huku zile za ugenini zikishinda minne wakati sare zikiwa mbili na kati ya hizo ametoa kadi za njano 68 na nyekundu tatu.

Mwamuzi huyo amewahi kuichezesha mchezo wa Yanga wakati timu hiyo ilipoifunga Club Africain ya Tunisia bao 1-0 Novemba 9, mwaka jana na kufanikiwa kuiondosha hatua ya mtoano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kwa jumla ya 1-0.

Ushindi mkubwa ambao timu ya nyumbani ilishinda wakati Issa akichezesha ni ule wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyoifunga Al Ahly ya Misri mabao 5-2, Machi 11, mwaka huu.

Naye Abongile Tom kutoka Afrika ya Kusini atakayechezesha mechi ya Yanga dhidi ya Rivers United atakuwa miungoni mwa waamuzi watakaochezesha Kombe la Dunia kwa vijana.

Rekodi za Abongile zinaonyesha katika michezo minane ya kimataifa aliyochezesha timu za nyumbani zimeshinda mechi tano huku za ugenini zikishinda mitatu na kati ya hizo ametoa kadi za njano 38 na nyekundu moja.

Miongoni mwa michezo aliyochezesha Abongile ni pamoja na ule wa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya De Agosto ya Angola, Oktoba 16, mwaka jana na kufuzu hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 4-1.

Chanzo: Mwanaspoti