Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WPL ni mastraika tu

GBy8tCBXEAAn0G WPL ni mastraika tu

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kule kwenye Ligi Kuu ya wanaume, vinara wa mabao ni viungo, lakini huku ligi ya wanawake, mastraika wameamua kumaliza jambo lao wenyewe.

Aziz KI wa Yanga na Feisal Salum wa Azam FC ndio wanaongoza wakiwa na mabao 13 kila mmoja lakini huku WPL kinara ni Asha Mnunka wa Simba Queens mwenye mabao 11 akifuatiwa na Stumai Abdallah wa JKT mwenye mabao 10.

Mastraika wengine ni Winifrida Gerald (JKT Queens) aliyefunga mabao saba, Asha Djafar (Simba Queens) mabao sita na Jentrix Shikangwa (Simba Queens), Janet Matulanga (Ceasiaa Queens) na Amina Ramadhan (Fountain Princess) waliofunga manne-manne kila mmoja.

Kwenye orodha ya Ligi Kuu ni mastraika watatu ambao wanashindana juu kwenye ufungaji bora, Waziri Junior wa KMC mwenye mabao 11, Samson Mbangula wa Tanzania Prisons (8), Adam Adam wa Mashujaa (7) na Prince Dube (7).

Katika WPL viungo wenye mabao mengi ni Vivian Corazone wa Simba Queens, Kaeda Wilson wa Yanga Princess na Donisia Minja wa JKT Queens ambao wamefunga mabao matatu-matatu kila mmoja

Chanzo: Mwanaspoti