Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WACHEZAJI WATATA: Ukiwapita, wakikupita lazima kadi itahusika

32046 Pic+watata TanzaniaWeb

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ligi Kuu Bara huwa na mvuto na vitimbi vya hapa na pale hasa wachezaji wakiwa uwanjani kuwania pointi tatu.

Katika kila sehemu kuna baadhi ya watu hao wapole na wengine huwa watata sana.

Utata huu huwa unakuja kwa mtu kuamua tu kuwa mbabe lakini wengine huwa watata pindi wakichokozwa.

Spoti Mikiki limefanya uchunguzi na kugundua kuwa wachezaji wengi watata kwenye Ligi Kuu Bara ni mabeki na hiyo inatokana na kushindwa kukubali kupitwa kirahisi na washambuliaji wa timu pinzani.

Mwananchi linakuletea wachezaji watata uwanjani ambao wanashindwa kuzuia hasira zao pindi wanapokorofishwa au huwa ni wepesi kununua usiowahusu.

Aggrey Morris- Azam

Beki huyu wa Azam amekuwa na matukio mengi hasa kupiga viwiko wenzake pindi wanapowania mipira hasa ya juu. Aliwahikumpiga kiwiko Emmanuel Okwi wa Simba katika mchezo baina yao uliofanyika Janauri 25 mwaka 2-15.

Alisabbaisha Okwi kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali hata hivyo na yeye alifungiwa mechi tatu. Mara kwa mara amekuwa akipata kadi z njano kutokana na kuchea rafu nyingi uwanjani.

Kelvin Yondani-Yanga

Mmoja wa mabeki bora kwa sasa hapa nchini lakini huwa hana masihara anapokuwa katika kazi yake uwanjani.

Wachezaji wengi wamekuwa wakimuogopa kutokana na utata wake kwani huwa hakubali ksuhindwa, ukimkorofisha lazima akurudishie tena anakurudishia kiaina hata mwamuzi anaweza asione.

Amewahi kufungiwa mechi tatu na faini ya sh 500,000 kwa kosa la kumpiga na boksi la dawa daktari wa Coastal Union Mganga Kitambi katika mechi kati ya Yanga na Coastal Union iliyofanyika Januari 30 mwaka 2016 uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Yondani alifanya kitendo hicho baada ya kunyimwa maji na daktari huyo.

Pia Mei mwaka huu aliiingia matatani baada ya camera za Azam Tv kumnasa akimtemea mate usoni beki wa Simba Asante Kwasi katika mchezo wa watani wa jadi ambao Simba ilishinda bao 1-0.

Juuko Murshid - Simba

Beki wa kati raia wa Uganda ambaye huwa ni mtata awapo uwanjani kutokana na kupiga soka la kibabe kwani huwa hakubali kupitwa kirahisi. Ana makosa ya mara kwa mara yanayosababishaga aonyeshwe kadi za njano.

Aliwahi kupata kadi nyekundu Februari 15 mwaka huu baada ya kumpiga kiwiko

Paul John wa Mwadui wakati wakiwani mpira.Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kambarage Shinyanga timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Donald Ngoma - Azam

Mshambuliaji kutoka Zimbabwe ambaye aliicheza Yanga kwa mafanikio na sasa ametua Azam FC.

Ana hasira za karibu awapo uwanjani kwani hapendi kubughudhiwa ovyo na mabeki. Alionyeshwa kadi nyekundu Novemba 4 mwaka huu katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Azam ilishinda bao 1-0 huku yeye akifunga bao hilo la ushindi.

Andrew Vincent’Dante’-Yanga

Unaweza usimdhanie kama ukimuangalia kijuu juu kutokana na kuwa na sura ya upole lakini matukio yake ya mfululizo ya hivi karibuni yanamuingiza katika kundi hili la wachezaji watata.

Septemba 30 alipatikana na hatia ya kumpiga kichwa beki wa Simba, Mohammed

Hussein Tshabalala katika mchezo wa watani wa jadi uliomalizika kwa suluhu.

Pia anaweza kuingia matatani kwa kosa la kumpiga kichwa mwamuzi katika mchezo dhidi ya Prisons uliofanyika Desemba 3 kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya ambao Yanga ilishinda mabao 3-1.

Vincent alikasirishwa na kitedo cha mwamuzi kuwapa penalti Prisons. Baadae pia alitoka mbio na kutaka kumvaa tena mwamuzi katika tukio lililoibua vurugu baada ya Mrisho Ngassa kumpiga kichwa Hassan Kapalata

Juma Nyosso- Kagera Sugar

Huyu ndio usimchezee kabisaa kwani huwa harembi katika kurudisha mashambulizi.Mwaka 2015 aliwahi kufungiwa mechi nane na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)kwa kumtomasa mshambuliaji wa zamani wa Simba Elius Maguri.

Pia mwaka huo huo alifungiwa miaka miwili na fainali ya sh 2 milioni kwa kumdhalilisha aliyekuwa mshambuliaji wa Azam John Bocco. Halafu Januari mwaka huu amewahi kukamatwa na jeshi la Polisi baada ya kumpiga shabiki wa Simba kwa madai alimpulizia vuvuzela masikioni wakati akifurahia ushindi wa Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar

Razack Abarola- Azam

Kipa Mghana wa Azam ambaye ana hasira kweli kweli awapo uwanjani. Mara nyingi amekuwa akiingia matatizoni na waamuzi kwani huwa haogopi kuwavaa pale anapohisi timu yake imeonewa.

Machi mwaka huu alifungiwa mechi tatu na Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kumtolea lugha chafu mwamuzi Jonesia Rukyaa baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Simba uliomalika kwa wekundu wa Msimbazi kushinda Nurdin Chona- Prisons

Beki mwingine mtata kwenye Ligi Kuu Bara. Amekuwa hana masihara uwanjani na hapendi kuona mchezaji wa timu yake anaonewa.

Abdallah Mfuko- Ndanda

Beki wa zamani wa Mwadui ambaye kwa sasa anaichezea Ndada ya Mtwara.Ni mtata kweli kweli kwani hawezi kucheza michezo mitatu mfululizo bila kuonyeshwa kadi ya njano.



Chanzo: mwananchi.co.tz