Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vurugu zaiponza Singida, Coastal zalimwa faini

Singida Vs Coastal Vurugu zaiponza Singida, Coastal zalimwa faini

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeitoza faini ya sh1 milioni Singida Fountain Gate kwa kosa la kuvamia Uwanja wa Liti wakati wa mazoezi ya mwisho ya Coastal Union siku moja kabla ya mchezo baina ya timu hizo na kusababisha vurugu.

Mbali na klabu kupigwa faini pia kamati imewatoza faini baadhi ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Singida.

Wliopigwa faini ni kipa Beno Kakolanya aliyefungiwa kucheza mechi tatu na faini ya Sh1 milioni kwa kumtolea lugha chafu kiongozi wa Coastal Union, Juma kindo huku kocha msaidizi wa timu hiyo, Thabo senong akifungiwa mechi tatu na faini ya sh1 milioni na Deus Kaseke na Hamad Waziri wametozwa faini ya Sh500,000 kwa kushiriki vurugu hizo na kuwatolea lugha mbaya viongozi wa Coastal.

Kwa upande wa Coastal, mchezaji Roland Beakou ametozwa faini ya Sh500,000 kwa kosa la kumwaga kimiminika katika mstari wa katikati ya uwanja baada ya ukaguzi wa kitendo kilichotafsiriwa kama Imani za kishirikina.

Chanzo: Mwanaspoti