Leo January 15, 2018 Kampuni ya simu za mkononi nchini ya Vodacom Tanzania imemkabidhi kiungo wa Klabu ya Singida United Mudathir Yahya Tsh Milioni 1 na Tuzo kwa kuibuka Mchezaji Bora wa Mwezi November 2017 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Mudathir ametwaa Tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzake wawili, Beki Asante Kwasi kipindi akiwa Lipuli ya Iringa na mshambuliaji Danny Usengimana ambaye nae yupo Singida United, alioingia nao fainali ya kuwania nafasi hiyo.
Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Singida United kwa mwezi November ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Oktober hadi nafasi ya nne.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi hizo ikiwemo Dekoda kutoka Azam TV, Mudathir amesema “kikubwa ambacho kimebadilika na kimenifanya niibuke mchezaji bora ni kocha Hans kuniamini kwasababu mtu akikuamini unafanya kile ulichonacho kwa juhuzi zaidi”.
Ajali ya HIACE iliyoua 11 Kagera, aligonga Malori mawili.
Cyprian Musiba atangaza kumshitaki Tundu Lissu