Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vladimir atua Namungo

Namungoooo5215301457 Vladimir atua Namungo

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa kocha wa makipa wa Klabu Soka ya Yanga, Vladmir Niyonkuru ametangazwa rasmi kuwa kocha wa Magolikipa wa Klabu ya Namungo FC ya Tanzania.

Vladimir ambaye ni raia wa Burundi amejiunga na kikosi hicho kwa mkataba wa miaka miwili.

Kocha huyo amewahi kufanya kazi pamoja na Kocha Mkuu wa Namungo, Cedric Kaze ambaye nae ni raia wa Burundi, walifanya kazi Yanga SC.

Kaze anawavuta warundi wenzake klabuni hapo ili kurahisisha utendaji kazi wake kwa kufanya kazi na watu ambao anawafahamu kwa karibu na hii inaonyesha Ligi ya Tanzania inazidi kukua na kuyavutia mataifa mengine kuja kufanya kazi na vilabu vya Bongo.

Kocha mkuu wa klabu hiyo Cedric Kaze, golikipa Nahimana Jonathan na Beki Mukombozi Derrick wote ni raia wa Burundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live