Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanja 'vyaikosti' ligi kuu Tanzania bara, yashuka viwango

Amri Abeid Arusha Uwanjaaa Viwanja 'vyaikosti' ligi kuu Tanzania bara, yashuka viwango

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Wallace Karia ameweka wazi kuwa kuwepo kwa viwanja vibovu imepelekea kushuka kwa ubora wa viwango vya ubora vya ubora Ligi Kuu ya Tanzania kutoka namba tano hadi Sita kwa Afrika.

Hayo ameyabainisha leo mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa teknolojia ya usaidizi wa muamuzi kwa video VAR hafla iliyoandaliwa na kampuni ya azam media iliyobatizwa jina la azam TV expose, viwanja vya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Karia amesema kuwepo kwa udhamini wa Azam Media kumekuwa na faida na hasara baada ya kuonyesha baadhi ya mechi na zinazochezwa katika viwanja vibovu imechangia kushuka kwa viwango vya ligi ya Tanzania.

“Hatujuti kuingia makubaliano ya kimkataba na Azam Media kwa sababu imeweza kusaidia kuonekana kwa ubora wa ligi yetu lakini pia tumeshuka viwango vya ubora kwa sababu ya ubovu wa baadhi ya viwanja.

Hatutaweza kuvumilia au kuruhusu timu za ligi kuu kucheza mechi zao kwenye viwanja vibovu, tunahitaji msimu huu wa 2024/25 tunapanda katika viwango kurejea katika nafasi yetu ya tano,” amesema Karia.

Ameupongeza uongozi wa Manispaa ya Kinondoni (KMC) kwa juhudi zao za kufanikiwa kujenga uwanja ambao unaweza kutumika katika michezo ya ligi ya msimu mpya.

Karia amemuomba Waziri Mkuu na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kutoa maelekezo kwa viongozi wa mikoa mingine kuboresha viwanja vyao kama ilivyo kwa Mkwakwani, Tanga kwa kuwa viwanja vingi kumilikuwa na CCM.

“Viwanja ambavyo sio rafiki vinapunguza umri wa mchezaji kwa kucheza kipindi kifupi, kama mchezaji anatakiwa kucheza miaka 20 basi hataweza kucheza na kukutana na majeraha kwa sababu ya ubovu wa uwanja na kulazimika kukaa nje kuuguza majeraha,” amesema Karia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live