Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanja vitatu kuwaka moto Ligi

Ratiba Leo Fgde Viwanja vitatu kuwaka moto Ligi

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja mbalimbali na mechi ya mapema saa 10:00 jioni itazikutanisha JKT Tanzania itakayoikaribisha Tabora United kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es Salaam.

JKT inaingia katika mchezo huo huku ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1, mechi yao iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons sawa na Tabora United ambayo nayo ililazimishwa suluhu na KMC kwenye Uwanja wake wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.

Mchezo mwingine utapigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani saa 12:30 jioni na ‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union ambayo bado haijaonja ladha ya ushindi msimu huu itaikaribisha Mashujaa iliyotoka kuchapwa bao 1-0 na JKT Tanzania mechi ya mwisho.

Mechi ya mwisho leo itapigwa saa 3:00 usiku na Dodoma Jiji iliyotoka sare ya mabao 2-2, mechi ya mwisho na Geita Gold itakuwa Uwanja wa Jamhuri kupambana na Kagera Sugar yenye kumbumbuku ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0.

Akizungumzia maandali ya mchezo huo kocha msaidizi wa Dodoma Jiji, Kassim Liogope alisema hautokuwa mchezo mwepesi kwao ingawa malengo yao ni kupata pointi tatu huku akiainisha wachezaji wote wako kwenye morali kubwa ya kupata ushindi.

“Tunahitaji kuendeleza rekodi nzuri katika uwanja wetu na hili tutalifanikisha kwa kuzingatia nidhamu ya kiuchezaji kuanzia uzuiaji na utumiaji wa nafasi vizuri kwa maana ya ushambuliaji, pointi tatu ndio malengo yetu makubwa,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti