Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanja Bongo tatizo, ila kwa Mkapa pasua kichwa

E0704F96 7869 4BFD BAA4 C3332F66054D.jpeg Viwanja Bongo tatizo, ila kwa Mkapa pasua kichwa

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2022/2023 ikianzabaadhi ya viwanja vilifungiwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa kukosa sifa ya kutumika kwa mechi za ligi hiyo.

Baadhi ya viwanja viliyofungiwa lakini baadaye vilifunguliwa ni Jamhuri-Dodoma, Ushirika-Moshi, Mkwakwani-Tanga, Highland Estate- Mbeyana Sheikh Amri Abeid- Arusha.

Jumla ya viwanja 18 hutumika kwenye mechi za Ligi Kuu ambavyo ni Benjamin Mkapa, Uhuru na Azam Complex vyote vya Dar es Salaam, Mabatini (Pwani), Sokoine na Highland Estate (Mbeya), CCM Kirumba (Mwanza), Sheikh Amri Abeid (Arusha), Ushirika (Moshi), Jamhuri Dodoma, Liti (Singida), Majaliwa na Ilulu (Lindi), Kaitaba (Kagera), Nyankumbu (Geita), Manungu (Morogoro) naMkwakwani (Tanga).

Pia, kuna viwanja 13 hutumika zaidi na mechi za Ligi ya Championship na First League ambavyo ni Meja Isamuhyo (Dar), Nangwanda (Mtwara), Jamhuri (Morogoro), CCM Gairo (Morogoro), Kambarage (Shinyanga), Nyamagana (Mwanza), Lake Tanganyika (Kigoma), Ali Hassan Mwinyi (Tabora), Gwambina Complex (Misungwi), Karume (Mara), Samora (Iringa), Majimaji (Songea) na Nelson Mandela (Sumbawanga).

Asilimia kubwa ya viwanja hivyo humilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo vilivyo vingi vimeonekana kutokuwa kwenye ubora unaostahili ingawa kwenye bajeti ya serikali mwaka huu ilitenga Sh 10 Bilioni kwa ajili ya ukarabati wa viwanja hivyo.

Baada ya fungiafungia hiyo Mwanaspoti linakuletea makala maalumu ambayo inaelezea viwanja vinavyotumika na ligi zote kuona namna vilivyo.

BENJAMINI MKAPA

Ni miongoni mwa viwanja bora vya soka barani Afrika na kwa mujibu wa Mtandao wa WikiPedia unashika nafasi ya 15 ukiwa na uwezo wa kuingiza watu 60,000. Ni uwanja ambao Simba na Yanga zinautumia kama uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi zao za ligi na zile za kimataifa.

Hata hivyo, licha ya uwanja huo kuonekana kuwa mkubwa umekuwa na changamoto nyingi hasa maeneo ya mifumo ya maji jambo linalosababisha pindi mvua ikinyesha wakati mwingine maji kutuama kwenye eneo la kuchezea (pitch).

Pia, kumekuwa na changamoto kubwa ya usafi wa vyoo na miundombinu ya vyoo hivyo kwenye uwanja huo kutokuwa vizuri na wakati mwingine kutotoa maji na kuwa vichafu.

Changamoto nyingine ni baadhi ya maeneo kuonekana kung’olewa viti na hata sehemu yenye viti kutofautina rangi halisi mfano kama ya kijani basi kutakuwa na kijani iliyokoza na nyingine iliyopauka huku pia kukionekana mashabiki wengi wakitumia sana mageti mawili tu licha ya uwanja kuwa na mageti mengi.

Mwanaspoti limehudhuria mechi mbalimbali uwanjani hapo na kushuhudiwa changamoto hizo, lilifanya mahojiano na Naibu Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Ally Mayay na aliyekuwa meneja wa uwanja huo kabla ya Waziri wa Michezo Mohamed Mchengerwa kufanya mabadiliko ya nafasi hiyo hivi karibuni, Daniel Madenyeka walizungumzia mambo mbalimbali na jinsi gani changamoto za uwanja huo zitatatuliwa.

IDADI YA MECHI

Madenyeka anasema Shirika la Ufundi la China ambalo ndilo limehusika kujenga uwanja huo linataka utumike kwa mechi zisizozidi mbili kwa wiki ili uendelee kuwa bora.

“Wametuambia walau kwa wiki mechi zichezwe mbili na kama ikizidi sana angalau tatu na lengo ni kuufanya uwanja kuendelea kuwa katika ubora wake.

“Wamepanga hivyo kwa kuangalia kama mechi zikichezwa wikiendi yaani Jumamosi na Jumapili ina maana Jumatatu hadi Ijumaa kunakuwa na muda wa kuweka uwanja vizuri ikiwemo kukata nyasi na kuboresha baadhi ya maeneo,” anasema Madenyeka aliyetolewa kwenye nafasi hiyo aliyokuwa akiikaimu baada ya Godwin Nsajigwa kutolewa Agosti mwaka huu.

Anasema wakati mwingine inabidi kuzidisha matumizi ya uwanja huo kutokana na mambo yaliyo nje ya uwezo wao mfano baadhi ya nchi kuomba kuutumia uwanja huo.

“Kuna muda uwanja unakuwa na matumizi makubwa tofauti na inavyotakiwa lakini sio kwamba tunapenda ila kuna mambo yanatokea unashindwa ufanyeje. Mfano kuna nchi zinaomba kutumia uwanja kucheza mechi zake na huwezi kuwakatalia.

“Hivi karibuni kulikuwa na mashindano ya Cambiasso na kuna timu ya Ufaransa ilipangwa icheza Uwanja wa Azam Complex wenye nyasi bandia lakini wakagoma wakasema hawawezi kucheza mechi wala kufanya mazoezi uwanja wa nyasi bandia sasa kwa hali hiyo unafanyaje,” anasema.

MSIKIE MAYAY

Anasema uwanja huo unatumika sana na wako kwenye mchakato wa kuandaa mwongozo wa uendeshaji wa uwanja huo.

“Huu ni uwanja wa nyasi za asili unatumika sana na kama unakumbuka mechi za kufuzu CHAN kuna mataifa ya jirani kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki, Sudan, Somalia, Rwanda na Burundi waliomba kucheza uwanja huu

“Unajua kuna viwango vya matumizi na namna ya kuutunza kwani nyasi za asili ni tofauti na nyasi bandia ndio maana kwa wenzetu uwanja kama Wembley uliopo London uko katika ubora uleule kwa zaidi ya miaka 40 kwa sababu wana mwongozo wa kuuendesha,” anasema Mayay.

Anasema hapa nchini jambo hilo ni moja ya changamoto inasababisha uwanja kupoteza ubora wake kwa sababu hakuna muongozo wa kiuendeshaji, ndio maana sasa hivi wako katika mchakato wa kuandaa muongozo wa uendeshaji wa uwanja hasa ile sehemu ya kuchezea pia mradi wa kuboresha miundombinu kuanzia kwenye viti na mifumo ya maji.

“Mfano wakati tukiwa India kwenye fainali za Kombe la Dunia la Wanawake U-17 kuna viwanja tulikuwa tunafanyia mazoezi, ikinyesha mvua kubwa hata kwa saa tatu, ndani ya dakika 20 tu maji yote yanatoweka, lakini yote ni kutokana na mifumo yao iko vizuri sasa nasi tumejipanga kuboresha jambo hilo la mifumo ya maji viwanjani

“Huo muongozo utashirikisha wadau hasa TFF ili hata mechi zitakavyokuwa zinapangwa itakuwa inajulikana kabisa kuwa baadhi ya siku kadhaa uwanja utakuwa unatumika au hautumiki.

“Tuko kwenye hatua za mwisho wa mchakato wa kupata tenda, tayari umeshaandaliwa na watu wameshaanza kutuma maombi na karibuni tutawapata wakandarasi,” anasema Mayay.

VYUMBA VYA MAREFA NA MADAKTARI

Madenyeka anasema Uwanja wa Mkapa ukiondoa vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji pia kuna chumba maalum cha matibabu endapo kutatokea tukio lolote la mchezaji, shabiki au kiongozi kupata tatizo la kiafya.

“Kuna vyumba vya dharura kwa ajili ya matibabu na madaktari wapo, ingawa kunakuwa na madaktari wa michezo katika mechi husika wanaokabidhiwa chumba ili ikitokea lolote wanamchukua mhusika na kumpeleka kwenye chumba hicho kwa ajili ya matibabu zaidi na ikishindikana kuna gari la wagonjwa linamchukua na kumwaisha hospitali.

Pia, kuna vyumba vya waamuzi vyenye meza na viti na baadhi ya vitu ambavyo ni maalumu kwa ajili ya waamuzi ikiwemo vyoo na mabafu

“Kwa hapa kwetu vyumba vya waamuzi vina baadhi ya vitu ingawa kuna sehemu kwa wenzetu unakuta vyumba hivyo vina Tv kabisa, ili kama kuna maelekezo wanapeana lakini hapa hatujawahi kupata maombi hayo kutoka kwa wahusika.

“Mfano kunapokuwa na mechi za kimataifa hapa unakuta waamuzi wanataka chumba chao kiwe na mtandao (internet), printa yaani chumba kiwe na kila kitu ili kama kuna chochote wanataka kutuma basi waweze kufanya kazi yao ipasavyo, ingawa vitu vyote hivyo mwenyeji wa mechi hiyo ndio anahakikisha vinakuwepo,” anasema.

MSIKIE MENEJA MPYA

Naye Meneja Mpya wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Salum Mtumbuka alisema; “Uchafu ulioonekana kwenye mitandao ya kijamii kwenye uwanja huu ulisababishwa na lile Tamasha la Mwamposa, kampuni ya usafi inayofanya usafi uwanjani hapo ilikusanya uchafu wote lakini walisahau kuubeba huo.

“Hata sisi hatukujua ila baadaye tuliwasiliana na hiyo kampuni na walienda kuutoa, upande wa miundombinu ya vyoo ni changamoto kutokana na uwingi wa watu wanaoingia uwanjani hapo lakini tumeliwasilisha kwa viongozi wetu na mkakati wa kulitatua hili umeanza,” anasema na kuongeza;

“Na hivi sasa, mechi inapomalizika kuchezwa lile eneo la kuchezea (pitch) linaanza kumwagiliwa maji, ili kuendelea kuutunza vizuri.”

UHARIBIFU WA VITI

Hapa Madenyeka analielezea; “Viti karibu vyote tunapewa msaada na China ambao ndio waliojenga uwanja huku kila mwaka wanaandika mahitaji yao kutoka katika serikali yao na wakati mwingine wanatuletea viti hivyo tunatoa vile vibovu na kuviweka vipya na wakati mwingine vile ambavyo havijaharibika sana tunavifanyia marekebisho.

Chanzo: Mwanaspoti