Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanja 16 kujengwa Zanzibar

Uwanja Wa Amaan ZNZ KKK.jpeg Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Dar24

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imepanga kujenga viwanja 16 vya michezo vya kisasa, ambavyo vitatumika wakati wa mchana na usiku.

Kauli hiyo ilitolewa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Abdullah amesema Serikali imepanga kulitumia eneo la Maisara kujenga viwanja vya michezo ambavyo vitatunika katika michezo ya aina mbalimbali.

Tunaanini kuwepo kwa viwanja hivi itasaidia kuibua vipaji zaidi vya vijana wetu kwa kila mchezo na kufanya vizuri kwa klabu na tinu zetu katika mashindano ya ndani na ya kimataifa,” amesema

Amesema mbali ya kuwa michezo ni sehemu ya burudani, pia ni njia moja wapo ya kuwapatia vipato vijana.

Pia, amesema michezo inajenga afya ya mwili na akili, hivyo kwa kuthamini yote hayo, SMZ itaendelea kuimarisha miundombinu ya viwanja vya michezo kukidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya wanamichezo.

Amesisitiza kuwa, Serikali imefanya matengenezo makubwa ya Uwanja wa New Amaan Complex (Unguja) na Uwanja wa Gombani (Pemba) pamoja na kujenga Uwanja mpya wa kisasa Matumbaku (Unguja).

Chanzo: Dar24