Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwango vya wachezaji Simba, Gomes kicheko

E9kwzaIXMAIBL1p Wachezaji wa Simba SC

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa maandalizi ya msimu ujao yanakwenda vizuri huku akifurahishwa na uwezo wa wachezaji ambao wanauonyesha.

Mchezo mmoja wa kirafiki Gomes aliwaongoza vijana yake ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya FAR Rabat ya Morocco ambapo ulikamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Baadhi ya wachezaji wa Simba wameondoka kambini na kujiunga na timu za taifa huku baadhi wakiendelea kuwa na kambi nchini Morocco na miongoni mwa nyota hao ni Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Chris Mugalu, Ally Salim.

Raia huyo wa Ufaransa amesema "Kila kitu kina kwenda sawa na maandalizi yapo vizuri jambo ambalo linaleta matumaini kwa ajili ya msimu mpya.

"Kila mchezaji anatimiza majukumu yake na hilo ni jambo la msingi hivyo imani yetu ni kuona kwamba tunakuwa na wakati mzuri kwa wakati ujao," .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live