Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwango vimeshuka au mfumo umewatema?

Hjdfhwvf Viwango vimeshuka au mfumo umewatema?

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rudi msimu wa 2022/2023, Kikosi kilichoshinda ubingwa wa Ligi kuu msimu wa 2022/23 Ubavu wa kulia alikuwa mali ya Kibwana Shomari na mara kadhaa alikula mbavu ya kushoto , Farid Mussa alipewa pia ubavu wa kushoto au winga kulingana na namna Nabi alivyoamka ,kwa Sure Boy yeye pale kati alianza kujenga utawala wake na Doctor Khalid Aucho.

Kikosi kilichotwaa ubingwa wa FA hivyo hivyo na hata kikosi kilichoifikisha Yanga fainali ya CAFCC wafia timu walikuwa hawa .

Nimewataja hawa kwa sababu walikuwa wanapata sana nafasi ili iwe rahisi kujadili na kuelewana.

2023|24 ,Benchi linaongozwa na Gamondi ambaye amekuja na usajili kwenye baadhi ya nafasi ,vijana hawa pichani kazi yao imekuwa kufanya mazoezi na timu na kusafiri ili kukamilisha idadi ya wachezaji wanaosafiri na timu .

Baadhi yao huwaoni hata wakikaa benchi ,baadhi wanakaa benchi na kupewa dakika chache inapobidi .

Swali la kujiuliza hapa, viwango vimeshuka ,wameridhika au mfumo umewakataa kwa maana maingizo mapya ni daraja la juu kuwazidi ?

Hapa hakuna mlango wa lawama kwa maana anapokuja bora zaidi yako unatakiwa kujiboresha ili kuleta ushindani ,tulitazame na kulichambua kwa upande huo pia ili tuweze kupata muafaka nini kimewaweka kwenye mbao ndefu ?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: