Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viungo wa Yanga wanaifunika Simba nzima

Yanga Tano Pacome Maxi 191929 Viungo wa Yanga wanaifunika Simba nzima

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safu ya kiungo ya timu ya Yanga imeonekana kuwa mwiba kwa mabeki wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kufunga mabao mengi (mabao 38) kuliko mabao yote yaliyofungwa na wachezaji wa timu ya Simba (mabao 34).

Baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wao kinara, Fiston Mayele mwishoni mwa msimu uliopita, kocha mpya Miguel gamondi ametengeneza mfumo ambao unawategema zaidi viungo washambuliaji na mawinga kucheka na nyavu.

Kiungo wa Yanga, Stephaie Aziz Ki ndiye kinara wa ufungaji mabao mpaka sasa akiwa na mabao 12 na assists 7 kwenye mechi 13 alizocheza sawa kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' mwenye mabao 12 na assists 5 kwenye mechi 20.

Winga wa Yanga, Augustine Okrah raia wa Ghana aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo msimu huu, jana alifungua account yake ya mabao akiwa Young Africans SC kwenye Ligi Kuu ya NBC baada ya kufunga bao dhidi ya Ihefu huku akiwa na assists mbili alizozitoa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Polisi Tanzania.

Idara ya kiungo ya Yanga imefunga magoli (38) kati ya mabao 49 ambayo yamefungwa na wachezaji wote wa Yanga kwenye Ligi Kuu Tanzania bara (NBC) sawa na asilimia 77.55 ya mabao yote ya Yanga.

Mabao - ⚽ 12, assists 7 — Aziz Ki Mabao - ⚽ 09, assists 2 — Maxi Nzengeli Mabao - ⚽ 08, assists 1 — Mudathir Yahya Mabao - ⚽ 07, assists 4 — Pacome Zouzoua Mabao - ⚽ 01, assists 0 — Okrah Magic Mabao - ⚽ 01, assists 0 — Skudu Makudubela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: