Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vituko vya Morrison vyatua Uingereza

MORRISON Mateo Kovacic Vituko vya Morrison vyatua Uingereza

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Chelsea, Mateo Kovacic juzi ametenga anga soka na kugeuka gumzo katika uwanja wa Stamford Bridge -London nchini Uingereza baada ya mchezo uliohusisha Manchester United na Chelsea kumalizika kisha kuondoka uwanjani akiwa amevaa nguo ya ndani tu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliingia uwanjani, akichukua nafasi ya Marc Cucurella dakika ya 36. Inaripoti mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Cucurella alitolewa na Graham Potter kwani meneja huyo alionekana kutoridhika na kiwango cha Cucurella aliyekuwa akicheza nje ya nafasi yake kama benki wa kushoto kila mara.

Hata hivyo, Chelsea waliimarika zaidi baada ya kuingizwa kwa Kovacic, ambaye alionekana kuhimili vema safu ya kiungo ya timu yake ambayo ilitoka sare ya 1-1 na mashetani hao wekundu.

Mashabiki walikuwa wakimshangilia kila mara kuashiria kumkubali Mcroatia huyo kwenye mchezo huo lakini mazungumzo yalibadilika haraka hadi kuelekea kwenye mbwembwe zake fupi alipokuwa akiondoka uwanjani.

Video zilizonaswa na kamera na kupakiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zilimuonesha kiungo huyo akikimbia kwenye kuelekea kwenye vyumba vya uwanja huo huku akiwa amevaa nguo ya ndani pekee.

Kwa kawaida, wachezaji huwa wanatoa jezi zao kwa mashabiki baada ya michezo, lakini inaonekana Kovacic (28), alienda mbali zaidi. Na hili limetajwa kuwa tukio jipya kuwahi kuonekana Barani ulaya hasa ikizingatiwa kwa upande wa Tanzania ilishawahi kushuhudiwa kituko cha aina hiyo.

Alikuwa kiungo mshambuliaji wa Simba mwaka jana, Bernard Morisson raia wa Ghana ambaye alivua bukta yake na kuivaa kichwani kisha kubaki na nguo ya ndani pekee kuashiria kusherehekea kumfunga mtani wake Yanga.

Wakati Morisson akikumbana na adhabu ya kufungiwa mechi kadhaa kutokana na kitendo hicho, kwa upande wa kiungo wa Chelsea haijaarifiwa kama atapewa adhabu yoyote ama mamlaka husika zitalifumbia macho tukio hilo.

Kwa kawaida, mchezaji anapovua jezi uwanjani huwa analambishwa kandi ya njano, je hili tukio la Kovacic adhabu yake itakuwa nini? Ama litafumbiwa macho kutokana na dhana kwamba lilitokea baada wa kipenga cha mwisho?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live