Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vito Mannone: Ramsdale ondoka Arsenal

Skysports Ramsdale Arsenal 5484905 Golikipa wa Arsenal Aaron Ramsdale

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Mlinda Lango wa Arsenal Aaron Ramsdale ameambiwa akusanye virago vyake na aondoke wakati wa dirisha la uhamisho wa Januari litakapofunguliwa ili kwenda kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kucheza.

Hayo yalisemwa na aliyekuwa kipa wa zamani wa Arsenal, Vito Mannone, ambaye pia aliwahi kukutana na nyakati ngumu kama zinazomtokea Ramsdale kwa sasa wakati alipokuwa na miamba hiyo ya Emirates.

Mannone wakati yupo Emirates alikuwa chaguo la pili nyuma ya kipa Wojciech Szczesny, lakini aliona inatosha na kuamua kutimkia zake Sunderland mwaka 2013.

Sasa kipa huyo Mtaliano anamwambia Ramsdale atumie vyema akili yake kama mwenzake David Raya ataendelea kupewa nafasi na kipa Mikel Arteta kwenye chaguo la kwanza la kipa wa kikosi hicho. Vito Mannone – A Safe Pair of Hands

Kipa wa Lille, Mannone, mwenye umri wa miaka 35, kwa sasa, alisema: “Si kitu rahisi, lakini Ramsdale yupo kwenye hali ambayo mimi nilichukulia ni mbaya sana. Namshauri apambane.

“Nilisubiri miaka minane kabla ya kuwa panga pangua kwenye Ligi Kuu England, Emi Martinez alisubiri kwa miaka 10 kabla ya kukamatia shoo. Lakini, Ramsdale nyakati zake hazijirudii, anapaswa kuondoka. Hana machaguo mengi anayoweza kufanya.”

Raya alinaswa kwa mkopo kutoka Brentford dirisha lililopita la kiangazi licha ya Ramsdale kuwa kwenye kiwango bora kabisa huko Arsenal.

Kocha Arteta anampendelea Raya kutokana na uwezo wake wa kuucheza mpira kwa miguu na amemtumia katika kila mechi.

Arsenal ipo kwenye mbio za ubingwa, lakini Mannone hawaamini kabisa wababe hao kama wataweza kuchukua ubingwa, akisema: “Arsenal siku zote inaoongoza ligi wakati wa Krismasi, lakini inakwenda kutibua. Nimeshuhudia hilo mara nyingi, hata nyakati zangu nilipokuwa kwenye ile timu.”

Chanzo: Dar24