Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vital O' mbioni kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Burundi

Vitalo Fc 1 Vital O' mbioni kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Burundi

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Vital’O FC imepata alama tatu muhimu baada ya kuichapa Messager Ngozi kwenye wiki ya 27 ya Ligi Kuu Burundi na kujiwekea njia nyeupe ya kubeba Kombe la Ligi Kuu Burundi msimu wa 2023/2024.

Bao la Vital’O FC limefungwa na mchezaji Alfani Bigirimana dakika ya 70 kwa mkwaju wa peneti na kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ikiwa na alama 68 mbele ya Flambea du Centre yenye alama 60.

Vital’O inahitaji alama tatu katika michezo mitatu iliyobaki ya Ligi Kuu Burundi na kuondoa ukame wa makombe baada ya mara ya mwisho kubeba kombe la Ligi Kuu msimu wa 2015/2016, miaka nane iliyopita.

Mchezo huo muhimu ulikuwa umesimamiwa na mwamuzi wa Kimataifa wa Burundi Pacifique Ndabihawenimana ambaye pia ndiye atakayesimamia mchezo wa nusu fainali kati ya TP Mazembe na Al Ahly klabu bingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live