Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vital'O: Tumekuja kuitoa Yanga

VitalO  Yanga Viongozi wa Vital’O

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa timu ya Vital’O ya Burundi, Arsene Bucuti amesema wamekuja nchini kuitoa Yanga SC katika Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Vital’O imepangwa kucheza na Yanga SC katika Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika na mchezo huo utafanyika Jumamosi katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Arsene alisema wanaiheshimu Yanga SC, lakini hiyo haiwafanyi waihofie na wamekuja Tanzania kwa ajili ya kazi hiyo ya kuwatoa kwa kuwa wameifuatilia vyema.

“Tumekuja hapa kwa kazi moja tu. Kuwatoa Yanga SC. Tuna kila kitu ambacho wao wameshinda. Hatutishiko nao.

“Tumewafuatilia katika michezo yote ambayo wamecheza kule Afrika Kusini hadi hapa Tanzania, hivyo tunaenda kucheza na timu tunayoifahamu vyema “ Yanga ina mashabiki Burundi?

"Ndiyo, Yanga SC ina mashabiki wengi Burundi kutokana na wachezaji Ammis Tambwe, Saidoo Ntibazonkiza na Didier Kavumbagu kuwahi kuitumikia timu hiyo," amesema Arsene Bucuti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live