Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya wababe nusu fainali Kagame Cup

KAGAME CUP SEMI F Mechi za nusu fainali Kagame cup kuchezwa wiki hii

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Michuano ya Vilabu Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Kagame Cup 2021 yanaingia hatua ya nusu fainali Jumanne hii jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, Express FC ambao waliongoza Kundi A watakabiliana na vijana wa KMKM SC kutoka Zanzibar katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali siku ya Jumanne Agosti 10, majira ya saa moja usiku (1:00) kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Jumamosi iliyopita Express iliwaadhibu wenyeji Young Africans SC 3-1 na kuwanyima tiketi ya kuingia kwenye hatua ya mtoano, wakati KMKM SC pia iliifunga Azam FC 3-2 katika mechi ya Kundi B.

Tumeamua na kuhamasishwa kushinda Kombe hili la CECAFA Kagame. Wachezaji wangu wameyapa uzito mashindano haya tangu mechi yetu ya kwanza, ”aliongeza Kocha Mkuu wa Express FC Wasswa Bbosa.

Katika mechi yao ya ufunguzi Express FC ilitoa kichapo kwa Atlabara FC ya Sudan Kusini kwa bao 1-0, kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Nyasa Big Bullets FC (Malawi).

Pambano la pili la nusu fainali litapigwa siku ya Jumatano Agosti 11 na litawakutanisha wawakilishi pekee wa Tanzania Bara Azam FC dhidi ya Nyasa Big Bullets katika pambano linalotarajiwa kuwa pambano gumu kutokana na viwango walivyoonyesha timu zote mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live