Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya viungo kiatu cha dhahabu

Vita Ya Viungo Kiatu Cha Dhahabu Vita ya viungo kiatu cha dhahabu

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Patashika za Ligi Kuu zinaendelea kushika kasi vita ya ubingwa inaendelea ambapo timu za Yanga SC, Azam FC na Simba SC zinatazamwa kama washindani wa taji hilo msimu huu.

Mbali na mbio za ubingwa utamu wa ligi hiyo namba sita kwa ubora Afrika umehamia katika kukisaka kiatu cha dhahabu ambapo ni vita ya viungo wawili waliowahi kukipiga katika timu moja Stephan Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum wa Azam FC.

Ni bao moja tuu linalowatofautisha nyota hao, Aziz Ki ana mabao 15 wakati Feitoto ameweka kambani mara 14. Aziz Ki amesaliwa na michezo nane wakati Feisal akibakisha michezo sita kabla ya kutamatisha msimu.

Wanaofuatia ni Waziri Junior wa KMC mwenye mabao 11, Max Nzengeli 09, Mudathiri Yahya 08 wote wa Yanga, Kipre Junior wa Azam Fc amefunga mabao nane.

Kuna kila dalili nyota hawa wakavuka idadi ya mabao yaliofungwa na washindi wa kiatu hicho msimu uliopita, Saido Ntibazonkiza na Fiston Mayele ambao walifunga mabao 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live