Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya usajili 2024/25 imeanza

Joshua Kimmich Furaha Joshua Kimmich

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: Dar24

Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wamepanga kuipiku Liverpool kwenye mchakato wa kuiwania saini ya kiungo wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Awali Liverpool ilikuwa ikitajwa kuwa na nafasi kubwa ya kumpata kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, kutokana na ukaribu uliopo kati yake na Kocha Jurgen Klopp lakini kuingia kwa Man City mambo huenda yakabadilika.

Tangu kuanza kwa msimu huu Kimmich mwenye umri wa miaka 29, amecheza mechi 29 za michuano yote.

Bayern inaonekana kuwa tayari kumuuza lakini ripoti zinaeleza inahitajika zaidi ya Pauni 40 milioni ili kumpata nyota huyo mwenye mkataba na timu hiyo hadi mwaka 2025.

Kumekuwa na timu nyingi kutoka England zinazohitaji huduma ya staa huyo kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Bayern.

Katika nyakati tofauti huduma ya staa huyo pia imewahi kuhitajika FC Barcelona ingawa changamoto imekuwa ni timu hiyo kutoweza kulipa kiasi cha pesa kinachohitajika ili kumsajili.

Chanzo: Dar24