Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya ufungaji Bora, nafasi ya pili hatima ni leo

Fei Aziz Ms Vita ya ufungaji Bora, nafasi ya pili hatima ni leo

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendawili cha timu itayoungana na Yanga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kitateguliwa leo wakati ligi inafikia tamati.

Azam na Simba zote zina pointi 66, lakini zinatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa Azam ikikusanya mabao 61 wakati Simba ina 57.

Timu yoyote kati ya hizo itakayofungwa au kutoka sare itacheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Lakini zikitoka sare Azam itanufaika na idadi kubwa ya mabao  na iwapo Simba haitashinda zaidi ya 6.

Katika vita ya mfungaji bora, Stephanie Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum wa Azam wote wana mabao 18 na ni michezo ya mwisho leo itakayoamua mchezji yupi atachukua kiatu cha dhahabu.

Vita ya kuepuka kushuka daraja imebaki kwa timu mbili, Tabora United yenye pointi 27 na Geita Gold yenye 25 wakati Kagera Sugar yenye pointi 31 italazimiaka kushinda mchezo ili kuepuka kucheza mtoani kubaki Ligi Kuu.

Michezo ya kumaliza ligi hiyo leo ni kama ifuatavyo:

Yanga vs Tanzania Prisons

Simba vs JKT Tanzania

Geita Gold vs Azam

Coastal Union vs KMC

Ihefu vs Mtibwa Sugar

Mashujaa vs Dodoma Jiji

Namungo vs Tabora United

Singida Big Stars vs Kagera Sugar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live