Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya namba moto uliwaka Ligi Kuu

Mayele X Diarra Vita ya namba moto uliwaka Ligi Kuu

Sat, 10 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yapo mengi yametokea kwenye Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika, Yanga imetetea taji, Simba imemaliza nafasi ya pili, huku Azam FC ikimaliza ya tatu ni kama ilivyokuwa uliopita wa 2021/22, timu hizo zilimaliza hivyo.

Ligi ilikuwa na ushindani wa aina yake, kulingana na ubora wa timu zilivyosajili, mashabiki walikuwa na wakati mzuri wa kufurahia burudani kwa kutazama mechi mbalimbali.

Hapa chini tunakuchambulia ndani ya vikosi vya Simba, Yanga na Azam FC namna ulivyokuwa ushindani wa namba baina ya wazawa na wageni ambao uliibua burudani kwa mashabiki kufurahia viwango vyao na kuwapa upana makocha kutoumiza akili mmoja akikosekana.

SAFU YA USHAMBULIAJI - YANGA

Japokuwa hakuna ubishi ndani ya kikosi cha Yanga, kinara wa mabao 16 Fiston Mayele alikuwa injini ya timu, kuna mzawa aliyepandishwa kikosi B Clement Mziza ambaye alikuwa akipewa nafasi anafunga, ana mabao manne kwenye Ligi Kuu na sita Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Baina yao haukuwa ushindani wa kuwania namba moja kwa moja,badala yake ni ushindani wa kutumia nafasi na ilimfanya kocha wao Nasreddine Nabi aendelee kuwaamini.

Ushindani mwingine ni wa mabeki wa pembeni Joyce Lomalisa na Kibwana Shomari ambao kila mmoja kwa zamu yake aliweza kuisaidia timu kufanya vizuri, Lomalisa alikuwa bora kupandisha mashambulizi, wakati Kibwana ilikuwa kwenye kukaba.

Kwa upande wa viungo wakabaji alikuwepo Khalid Aucho ambaye alifanya vizuri kwa upande wa wageni,lakini wazawa waliwakilishwa vyema na Salum Abubakar 'Sure Boy' na wengine wengi waliofanya vizuri.

Kila nafasi kocha Nabi alijaribu kuwapa nafasi mfano beki ya kati, kipindi ambacho nahodha Bakari Mwamnyeto yupo nje Aucho alikuwa anashuka kutoka sita kwenda kucheza namba tano, pia wazawa kwa wazawa baina ya Dickson Job akaanza kuchezeshwa Ibrahim Bacca.

Kwa upande wa kipa, Djigui Diarra hakuwa na mpinzani ingawa wazawa walipopewa nafasi mfano baada ya kusajiliwa Aboutwalib Mshery alidaka vizuri mechi za mwanzo,vivyo hivyo kwa Metacha Mnata aliingia dirisha dogo akitokea Polisi Tanzania.

SIMBA - KAPOMBE, TSHABALALA, MANULA

Kuna maeneo ambayo Simba wazawa wamejidhatiti, mfano beki za pembeni ambazo wakikosekana Shomari Kapombe(namba mbili) na nahodha msaidizi Mohamed Hussein 'Tshabalala'(namba tatu) kocha Robert Oliveira 'Robertinho' ilikuwa lazima akune kichwa.

Vivyo hivyo baada ya kuumia kipa namba moja, Aishi Manula ilizua presha kwa mashabiki hadi ikafikia hatua ya kumpa nafasi Ally Salim kudaka dhidi ya Ihefu, Yanga na Wydad, nalo lilikuwa eneo la wazawa pekee.

Tukirejea kwenye ushindani baina ya wazawa na wageni eneo la ushambuliaji Moses Phiri alianza na kasi kubwa kabla ya kupata majeraha ambapo alifunga mabao 10, walishindana na nahodha John Bocco ambaye ana mabao tisa.

Ushindani mwingine ulikuwa kwa viungo wakabaji ambapo wote walikuwa kwenye viwango vya kuisaidia timu ni baina ya mzawa Mzamiru Yassin na mgeni Sadio Kanoute.

KWA UPANDE WA AZAM FC

Kwenye safu ya ushambuliaji ya Azam FC kuna Idris Mbombo kwa upande wa wageni aliyeingia kwenye ushindani wa namba na wazawa ambao walikuwa wanapata nafasi kama Ayubu Lyanga,

Viungo Cleofas Mkandala na James Akaminko pamoja na Nado na Sapu wanaingia humo. Kwa upande wa mabeki wa timu hiyo wazawa ambao hawakuwa nyuma kuwania nafasi ni Abdallah Sebo, Nathanael Chilambo, Edward Manyama, Lusajo Mwaikenda, huku wageni wakiwa bruce kangwa, Pape Ndoye na Daniel Amoah.

Wakati makipa wageni wazawa ni Zuberi Foba na Wilbol Maseke huku wageni wakiwa Idrisu Abdulai na Ali Ahamada ambao wote walipata nafasi kwa nyakati tofauti.

Chanzo: Mwanaspoti