Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya namba Simba yamtesa Miraji

77662 Miraj+pic

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MAAJABU ya straika wa Simba, Miraji Athuman kutokea benchi na kufunga mabao mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu kumemuibua nyota huyo na kutoboa siri yake huku akisema ushindani wa namba kikosini unamtesa.

Nyota huyo wa zamani wa Toto Africans, Mwadui na Lipuli amefunga mabao mawili katika mechi tatu ambazo timu yake imecheza ambapo imekuwa ngumu kuwatoa wazoefu kama Meddie Kagere na John Bocco pamoja na Deo Kanda ingawa kocha Patrick Aussems humfanyia mabadiliko kwa kutegemea na mchezo ulivyo kwa mchezaji atakayemtoa.

Mshambuliaji huyo mwenye kasi uwanjani hayupo kikosi cha kwanza lakini anapotokea benchi huonyesha kiwango kikubwa ikiwemo kufunga mabao na kuwapa shwangwe mashabiki wake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Miraji alisema kasi yake ya ufungaji mabao inatokana na juhudi binafsi na kutambua kazi yake pamoja na kufuata maelekezo ya kocha wake.

Alisema licha ya juhudi zake lakini ishu ya ushindani wa namba kikosini unamuumiza kichwa na kwamba kuanzia benchi hawezi kuingilia mipango ya Benchi la Ufundi isipokuwa anasikiliza maamuzi yao.

“Kwanza nashukuru kwa kiwango nilichonacho na hii ni kutokana na kujituma ndani na nje ya uwanja, lakini siyo siri ushindani wa namba ni mkali sana na ndio maana nasikiliza maamuzi ya Kocha anavyoniamulia”alisema

Nyota huyo aliongeza kuwa moto walioanza nao anaona wazi dalili za Simba kutetea tena ubingwa wa Ligi Kuu huku akiweka wazi kuwa licha ya vita iliyopo wamejipanga kufanya vizuri.

Kuhusu mbio za ufungaji bora, Miraji huyo alisema kasi ya Meddie Kagere mwenye mabao matano inamtisha na amemtangulia lakini lolote linawezekana huko mbeleni.

“Ubingwa tunaweza kuuchukua tena, Ligi ni ngumu na ishu ya ufungaji bora, Kagere amenitangulia lakini lolote linaweza kutokea kikubwa ni kutokata tamaa”alisema nyota huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz