Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya kiatu cha dhahabu yazidi kunoga AFCON

Winner AFCON 2024 Vita ya kiatu cha dhahabu yazidi kunoga AFCON

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchakamchaka wa kusaka Kiatu cha Dhahabu kwenye fainali za Afcon 2023 unazidi kunoga wakati michuano hiyo ikiingia kwenye mechi za pili za hatua ya makundi.

Straika wa Cameroon, Vincent Aboubakar ndiye aliyeibuka mfungaji bora kwenye fainali za Afcon zilizopita, wakati alipofunga mabao manane mwaka 2021.   Lakini, safari hii kwenye Afcon 2023, majeraha yametibua ndoto zake za kugombea tuzo hiyo ya ufungaji bora na kuanza vita hiyo kupambaniwa na wakali wengine wakiwamo Victor Osimhen, Mohamed Salah na Sadio Mane ambao wamefunga mara moja kwenye mechi mbili za kwanza.   Lakini, kuna sapraizi kubwa kwenye mbio hizo za kusaka Kiatu cha Dhahabu, ambapo hadi kufikia juzi Jumamosi asubuhi, staa wa Equatorial Guinea, Emilio Nsue, ndiye aliyekuwa kinara baada ya kupachika nyavuni mabao matatu.

Fowadi huyo wa CF Intercity mwenye umri wa miaka 34, alifunga hat-trick katika mechi ya ushindi wa mabao 4-2 iliyopata Equatorial Guinea dhidi ya Guinea-Bissau, Alhamisi iliyopita katika mchezo wa Kundi A.

Wanaomfuatia kabla ya mechi za jana ni mkali wa Senegal, Lamine Camara, aliyefunga mabao mawili, kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi, wakati Simba wa Teranga ilipochapa Gambia.   Mohamed Kudus wa Ghana amefunga mara mbili kwenye fainali hizo, alipofanya hivyo kwenye mchezo wa sare ya mabao 2-2 iliyopata Black Stars mbele ya Misri katika mchezo wa pili wa Kundi B.   Mostafa Mohamed wa Misri ameingia kwenye orodha hiyo kuwania Kiatu cha Dhahabu, ambapo straika huyo amefunga mara mbili katika mechi mbili alizotumikia timu yake katika mchakamchaka wa Afcon 2023 kwa Kundi B.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live