Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya funga mwaka ipo hivi Ligi Kuu

Yanga Algeria Tiziiiiii Vita ya funga mwaka ipo hivi Ligi Kuu

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zimesalia wiki kama mbili tu kabla ya mwaka 2023 kufikia tamati na kukasirishwa 2024, huku Ligi Kuu Bara utamu ukizidi kunoga na kuacha maswali kwa wadau mwaka utafungwaje safari hii kutokana na hesabu za vigogo Simba, Yanga na Azam zinazochuana kwenye msimamo.

Kwa sasa Azam inaongoza ikiwa na pointi 28 baada ya mechi 12, huku Yanga ikifuata na alama 24 ikicheza mechi tisa, ilhali Simba ikiwa ya tano ikikusanya alama 19 kupitia mechi nane.

Mwanaspoti linakuchambulia michezo iliyobaki kwa Yanga, Simba na Azam FC na ni timu ipi itamaliza kibabe mwaka huu.

AZAM FC

Ushindi wa karibuni ilioupata Azam FC wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania umeifanya kujikita kileleni na pointi 28 baada ya michezo 12 huku ikimaliza mwaka dhidi ya Kagera Sugar Desemba 21.

Timu hiyo imekuwa kwenye kiwango bora kwani ushindi mbele ya JKT Tanzania umeifanya kushinda mechi tano mfululizo bila ya kufungwa huku mara ya mwisho ikiwa ni kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Namungo, Oktoba 27, mwaka huu.

Katika michezo hiyo iliyoshinda Azam imefunga mabao 18 ikiruhusu kufungwa mara mbili hivyo endapo itashindadhidi ya Kagera Sugar itamaliza mwaka huu ikiwa na pointi 31.

YANGA

Mabingwa hao watetezi wana kazi ya kufanya msimu huu kutetea ubingwa kwani hadi sasa wamecheza michezo tisa ambapo wameshinda minane na kupoteza mmoja huku wakikusanya pointi 24 nyuma ya Azam FC.

Michezo iliyosalia kwa Yanga kumaliza mwaka ni dhidi ya Mtibwa Sugar inayoburuza mkia Desemba 16 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Tabora United (Desemba 22) ugenini na kumalizia nyumbani na Kagera Sugar Desemba 26 na Mashujaa Desemba 29. Hadi hapo Yanga itamaliza ikiwa na michezo 13 na ikishinda yote itamaliza kinara na pointi 36.

SIMBA

Timu hiyo iko nafasi ya tano kwenye msimamo na pointi 19 ambapo kati ya hiyo imeshinda sita, sare mmoja na kupoteza mmoja.

Michezo iliyobaki Simba na Kagera Sugar (Desemba 15) nyumbani kisha ugenini dhidi ya KMC, Desemba 23, Mashujaa, Desemba 26 na Tabora United, Desemba 29 na ikiwa itashinda michezo yote minne itakuwa imekusanya pointi 31.

MSIMU ULIOPITA

Kwa timu hizo hadi mwaka 2022 unakwisha zilikuwa zimecheza zote michezo 19 ya Ligi Kuu Bara ambapo Azam ilishinda 12, sare minne na kupoteza mitatu ikivuna pointi 40 huku Simba ikishinda 13, sare tano na kupoteza mmoja ikakusanya pointi 44.

Kwa upande wa mabingwa watetezi Yanga ilishinda 16, sare miwili na kupoteza mmoja ikakusanya pointi 50.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live