Huko mtaani hadi sasa mjadala ni ishu ya Tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, baada ya Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibazonkiza wa Simba kufungana kwa kila mmoja kufunga mabao 17, huku Bodi ya Ligi (TPLB) ikishindwa kuainisha kanuni za msimu huu zinaamua jambo hilo.
Mashabiki wa Yanga wanaamini Mayele anastahili kubeba tuzo hiyo, huku wale wa Simba wakimpigia upatu Saido aliyesajiliwa Msimbazi katika dirisha dogo akitokea Geita Gold alikofunga mabao manne na kuasisti mara sita kabla ya kuongeza mabao mengine 13 na asisti sita pia akiwa na Wekundu.
Sasa kama hujui ni kwamba vita ya mastaa hao sasa imehamia kwenye tuzo za msimu zinazotarajiwa kutolewa leo jijini Tanga, hafla itakayofanyika mara baada ya mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itakayozikutanisha Yanga na Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini humo.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linalosimamia tuzo hiyo kupitia Kamati ya Tuzo imepeleka hafla hizo Tanga na kuipanga ifanyike muda mfupi tangu kupigwa kwa mechi hiyo ya fainali ya ASFC kutokana na muingiliano wa kalenda ya FIFA inayohusisha mechi za kimataifa kwa timu za taifa.
Baadhi ya nyota wa timu za Ligi Kuu walioitwa na timu zao wakiwamo wale wa Tanzania, Taifa Stars na nyota wa kigeni wanatakiwa kuwahi kambi za timu zao, kwa ajili ya mechi za raundi ya tano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazopigwa kati ya Juni 14-20.
Stars yenyewe inatarajiwa kuikaribisha Niger kwenye pambano litakalopigwa Juni 18 ambapo timu hiyo ya Tanzania inahitaji ushindi ili kujiweka pazuri kwa ajili ya kufuzu fainali hizo za Ivory Coast.
MAENEO MANNE MAGUMU
Achana ishu za mechi za kufuzu Afcon 2023, unaambiwa kwenye tuzo hizo za msimu huu ambao majina ya wanaowania yalitangazwa wiki kadhaa zilizopita kuna maeneo manne magumu ikiwamo kuibuka upya kwa vita ya Mayele na Saido kwenye vipengele viwili tofauti.
Vipengele vinne vinaonekana kutotabirika katika uwaniaji wa tuzo hizo za msimu huu, ambazo washindi wake watatangazwa leo ni ile ya Mchezaji Bora, Kiungo Bora, Beki Bora na ile ya Mfungaji Bora wa msimu vipengele vinne ambavyo vinaonekana kuteka hisia za wengi katika utoaji wa tuzo hizo msimu huu.
Kiwango bora kilichoonyeshwa na walioteuliwa kugombea ushindi wa tuzo, unafanya wengi wasubiri kwa hamu kuona nani watakaibuka washindi katika vipengele hivyo.
Vita kubwa inaonekana ipo katika tuzo ya mchezaji bora ambayo inawaniwa na Fiston Mayele na Djigui Diarra wa Yanga, Saido Ntibazonkiza na Mzamiru Yassin (Simba) na Bruno Gomes wa Singida Big Stars.
Mayele amekuwa na msimu bora ndani ya kikosi cha Yanga akiifungia mabao 17 yaliyochangia itwae ubingwa wakati Diarra amekuwa nguzo imara golini, akiongoza katika kucheza idadi kubwa ya mechi bila kuruhusu mabao.
Wakati Saido Ntibazonkiza akionyesha kiwango bora katika kufumania nyavu na kupiga pasi za mwisho akiwa amehusika na mabao 29 ambapo amefunga 17 na kupiga asisti 12, Mzamiru Yassin ameonyesha kiwango bora katika safu ya kiungo ya Simba.
Kwa upande wa Bruno, amekuwa uti aa mgongo wa Singida United hasa katika kuichezesha timu na kufunga mabao ambapo amepachika idadi ya mabao tisa.
Katika tuzo ya kiungo bora, Mzamiru, Bruno, Saido wakiungana na Clatous Chama na Aziz Ki watanogesha ushindani wa kuwania mshindi wa kipengele hicho.
Wakati Chama akibebwa na idadi kubwa ya pasi za mwisho ambapo amepiga 14, Aziz Ki anabebwa na mabao yake ambayo ni nane huku akipiga pasi za mwisho tatu.
Bakari Mwamnyeto na Dickson Job walioonyesha kiwango bora cha kuilinda timu katika kikosi cha Yanga msimu huu kilichoruhusu mabao 18, watakuwa wakiwania tuzo na Enock Inonga, Mohamed Hussien na Shomari Kapombe ambao wameiongoza timu yao kuruhusu mabao 17 pia.
Tuzo zingine ambazo zinaonekana zitakuwa zinapasua kichwa wengi na kuleta hamu ya kufahamu ni nani anaweza kuibuka mshindi ni ile ya mwamuzi bora na refa bora msaidizi, mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho la Azam, kamishina bora na mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake.
Djigui Diarra anaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi wa tuzo ya kipa bora kama ambavyo Omari Malule anaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa meneja bora wa uwanja.
TUZO ZILIVYO
KOMBE LA ASFC
KIPA BORA
Benedict Haule (Singida)
Djigui Diarra (Yanga)
Abdulai Iddrisu (Azam)
MCHEZAJI BORA
Prince Dube (Azam)
Fiston Mayele (Yanga)
Abdul Suleiman (Azam)
Bakari Mwamnyeto (Yanga)
Clement Mzize (Yanga)
MFUNGAJI BORA
Andrew Simchimba-7 (Ihefu, iliyotolewa)
Clement Mzize - 6 (Yanga)
Abdul Suleiman- 3 (Azam)
LIGI KUU WANAWAKE
KIPA BORA
Najiath Abbas (JKT Queens)
Winfrida Jedah (Fountain Princess)
Gelwa Yona (Simba Queens)
CHIPUKIZI BORA
Winfrida Charles (Alliance Girls)
Winfrida Gerald (Fountain Princess)
Jackline Shija (JKT Queens)
MCHEZAJI BORA
Donisya Minja (JKT Queens)
Jentrix Shikangwa (Simba Queens)
Amina Bilal (Yanga Princess)
KOCHA BORA
Ally Ally (JKT Queens)
Juma Hussein (Fountain Princess)
Charles Lukula (Simba Queens)
KIKOSI BORA
Kitatajwa leo
MFUNGAJI BORA
Jentrix Shikangwa (Simba Queens)
TIMU YENYE NIDHAMU
Amani Queens
JKT Queens
Alliance Queens
MWAMUZI BORA
Jonesia Rukyaa-Kagera
Tatu Malogo- Tanga
Esther Adalbert- Singida
MWAMUZI MSAIDIZI BORA
Janeth Balama- Iringa
Glory Tesha- Dar
Zawadi Yusuph- Dar
LIGI KUU BARA
MCHEZAJI BORA
Mzamiru Yassin (Simba)
Fiston Mayele (Yanga)
Bruno Gomes (Singida)
Djigui Diarra (Yanga)
Saido Ntibazonkiza (Geita/ Simba)
KIPA BORA
Aishi Manula (Simba)
Djigui Diarra (Yanga)
Benedict Haule (Singida)
BEKI BORA
Dickson Job (Yanga)
Henock Inonga (Simba)
Bakar Mwamnyeto (Yanga)
Shomari Kapombe (Simba)
Mohamed Hussein (Simba)
KIUNGO BORA
Bruno Gomes (Simba)
Mzamiru Yassin (Simba)
Stephane Aziz KI (Yanga)
Clatous Chama (Simba)
Saido Ntibazonkiza (Geita/Simba)
KOCHA BORA
Nasreddine Nabi (Yanga)
Hans Pluijm (Singida)
Roberto Oliveira (Simba)
MENEJA BORA UWANJA
Omari Malule (Highland Estate, Mbeya)
Hassan Simba (Liti, Singida)
Amri Juma (Azam Complex)
CHIPUKIZI BORA
Clement Mzize (Yanga)
Edmund John (Geita Gold)
Lameck Lawi (Coastal Union)
KIKOSI BORA
Kitatangazwa leo
TIMU YENYE NIDHAMU
KMC
Ruvu Shooting
Tanzania Prisons
MWAMUZI BORA
Jonesia Rukyaa (Kagera)
Tatu Malogo (Tanga)
Ramadhan Kayoko (Dar)
Mwamuzi Msaidizi Bora
Mohamed Mkono (Tanga)
Frank Komba (Dar)
Janeth Balama (Iringa)
SETI BORA WAAMUZI
Simba v Yanga
Jonesia Rukyaa
Mohamed Mkono
Janeth Balama
Tatu Malogo
Simba v Azam
Abdi wajihi
Arnold Bugado
Martin Mwalyaje
Isihaka Mwalile
Geita Gold v Dodoma Jiji
Jonesia Rukyaa
Zawadi Yusuph
Athuman Rajabu
Ally Simba
KAMISHNA BORA
Isaac Munisi
Hosea Lugano
Said Mankilingo
MCHEZO WA KIUNGWANA
Saido Ntibazonkiza (Geita/ Simba)
Jean Baleke (Simba)
Pape Ousmane Sakho (Simba)
BAO BORA
Litafahamika leo
MFUNGAJI BORA
Fiston Mayele-17 (Yanga)
Saido Ntibazonkiza- 17(Geita/Simba)
TUZO ZA UTAWALA
TUZO YA HESHIMA YA WPL
Mshindi atatangazwa leo
MCHEZAJI GWIJI
Mshindi atatangazwa leo
TUZO YA HESHIMA
Mshindi atatangazwa leo
TUZO YA RAIS
Mshindi atatangazwa siku ya sherehe
LIGI NYINGINE
Mchezaji Bora Championship
Edward Songo (JKT Tanzania)
John Budeba (Mashujaa)
Fabrice Ngoy (Kitayosce)
MCHEZAJI BORA FIRST LEAGUE
Ramadhan Athuman (Rhino Rangers)
Abdulrahman Mapande (Cosmopolitan)
Tungu Kashinje (Stand United)
MCHEZAJI BORA U20
Lamdaki Chasambi (Mtibwa Sugar)
William Mwani (Mbeya Kwanza)
Clement Mzize (Yanga)
MCHEZAJI BORA SOKA UFUKWENI
Ligi bado haijachezwa
WASHINDI MSIMU ULIOPITA
MCHEZAJI BORA
Yannick Bangala (Yanga)
KIUNGO BORA
Yannick Bangala (Yanga)
KIPA BORA
Djigui Diarra (Yanga)
MFUNGAJI BORA
George Mpole (Geita Gold)
BEKI BORA
Henock Inonga (Simba)
Mwanaspoti. Kata k