Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya Ligi Kuu Bara yarudi upya

NBC Premier League Logo Pdf Vita ya Ligi Kuu Bara yarudi upya

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Utamu umerudi. Ligi Kuu Bara inaingia raundi ya sita leo kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Mtibwa Sugar iliyoachana na kocha Habib Kondo itakayoikaribisha Kagera Sugra kwenye pambano la ‘Tamtam Derby’ litakalopigwa Uwanja wa Manungu Complex, mkoani Morogoro kuanzia saa 10:00 jioni.

Ligi ilisimama kwa wiki mbili ili kupisha kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kwa mechji za timu za taifa, huku ikiwa imepigwa mechi za raundi tano na Simba ikiwa kileleni na pointi 15, ikifuatiwa na Azam yenye 13 kisha Yanga ikiwa imekusanya alama 12 na sasa leo inarudi kwa dabi hiyo ya walima miwa.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha msaidizi wa Mtibwa, Awadh Juma ‘Maniche’ alisema kwa sasa hali ya kikosi hicho ni nzuri huku akiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tumejiandaa kwa ajili ya mchezo huo. Ni kweli hatuna mwanzo mzuri ila bado tuna nafasi ya kurekebisha kasoro zilizopo ili kurejesha morali ya timu kiujumla,” alisema kocha huyo.

Kwa upande wa kocha wa Kagera, Mecky Maxime alisema wiki mbili zimetosha kutengeneza balansi kwenye timu hususan katika eneo la ulinzi na ushambuliaji.

“Kila mchezo ni mgumu kama ilivyokuwa mingine iliyopita ila tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya, wiki mbili kwetu zimekuwa na athari nzuri kwa sababu tumetumia maeneo mawili ya ulinzi na ushambuliaji kuyarekebisha,” alisema Maxime.

Mtibwa ambayo haijaonja ladha ya ushindi tangu msimu huu uanze inakutana na Kagera huku ikiwa na rekodi nzuri kwani mara ya mwisho zilipokutana ilishinda mabao 3-0, Juni 6, mwaka huu katika mchezo uliopigwa pia kwenye Uwanja wa Manungu.

Chanzo: Mwanaspoti