Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya Dabo na Mgunda bado inaendelea

Dabo Azam 128.png Vita ya Dabo na Mgunda bado inaendelea

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu Azam FC, Youssouph Dabo amesema kuwa malengo yake ni kuhakikisha anashinda michezo yote mitatu iliyosalia ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza wa pili kwenye msimamo wa ligi.

Dabo amesema hayo baada ya Simba ambao wanawania nao nafasi ya pili ili kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao kudondosha alama mbele ya Kagera Sugar na kufanya walingane kwenye alama iwapo wote watashinda michezo yao iliyosalia huku Azam akiwa na faida ya idadi kubwa ya tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

"Bado nina kazi kubwa ya kufanya katika mechi zangu tatu zilizobakia, nahitaji kupata ushindi katika mechi hizo ili kufanikisha hilo, natakiwa kuongeza nguvu kubwa kwa wachezaji kwa kuwaongezea mbinu zaidi.

“Mechi za mwishoni mwa msimu mara nyingi huwa ngumu, hivyo nitaendelea kutoa mbinu mpya kwa kikosi changu kupata ushindi. Lengo langu kubwa ni kuiona timu yangu ikimaliza katika nafasi za juu, hivyo tutapambana kushinda kila mechi,” amesema Dabo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live