Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya Aziz KI, Fei Toto yahamia Ligi ya wanawake

Aisha Mnunka Aisha Mnunka

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Achana na ubingwa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) uliobebwa na Simba Queens, unaambiwa ligi hiyo haijaisha kwenye vita ya kimya kimya ya kuwania kiatu cha Mfungaji Bora wa msimu huu.

Kama ilivyokuwa Ligi Kuu Bara kwa Mfungaji Bora kupatikana katikae mechi za mwisho, ndivyo ilivyo kwa WPL ambayo mechi mbili zilizosalia kabla ya kufungia msimu zitaamua nani anaondoka na kiatu.

Katika Ligi Kuu Bara kwa Wanaume, Stephane Aziz KI wa Yanga alimpiku dakika ya mwishoni Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam waliokuwa wanachuana.

Aziz KI alimaliza na mabao 21 na Fei Toto alifunga 19 akimaliza wa pili.

Mbali na ushindani wa timu hizo kuwania mataji ya WPL lakini pia msimu huu wachezaji wa Simba na JKT Queens kuna wana vita ya kupachika mabao.

Hadi sasa Aisha Mnunka wa Simba ndiye anayeongoza kama kinara wa mabao akiwa na mabao 19 akifuatiwa na Stumai Abdallah mwenye nayo 18.

Ukiachana na wawili hao wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua kiatu kutokana na idadi kubwa ya mabao waliofunga lakini kuna Jentrix Shikangwa (Simba Queens) aliyeweka kambani mabao 11 na Winifrida Gerald (JKT Queens) aliyefunga mabao 10.

Chanzo: Mwanaspoti